Kamatimu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kamatimu kati ya Wagikuyu ni jina la wanaume ambao bado hawajajiunga na jamii ya wazee, adhuri.

Sherehe maarufu ya "Mburi ya Kiama" huwa fursa ya Kamatimu kuoredheshwa kama mzee. Katika sherehe hizi mbuzi wawili huchinjwa kama ishara ya ombi na kafara kwa niaba ya Kamatimu. Sherehe hii ni maarufu eneo la katikati ya Kenya na haswa hufanyika mahala ambako kuna msitu. Hii ni baadhi ya tamaduni zilizohifadhiwa.

Kwa kawaida kamatimu anaweza kujiunga na wengine kwenye sherehe lakini kuna mengi asiyoweza kuyafanya. Mojawapo ya haya ni, hana uwezo wa kushirikishwa kwenye kikao cha kutoa maamuzi yanayohusiana na jamii.

Makala hii kuhusu utamaduni wa Kenya bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kamatimu kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.