Irene Kiwia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Irene Kiwia ni mwanaharakati na mjasiriamali nchini Tanzania,alizaliwa tarehe 14 Januari 1980 jijini Arusha. Pia ni mwanzilishi na mkurugenzi mtendaji katika shirika la "Frontline Porter Novelli (FPN)" tangu mwaka 2006.[1]

Maisha Yake[hariri | hariri chanzo]

Irene ni mtoto wa kwanza katika familia yenye watoto sita.Wazazi wake walitengana akiwa na umri mdogo na kulelewa na baba yake mzazi Mzee Elias Dawson Kiwia. Irene pia ni mama wa watoto wa kiume watatu Zion,Ethan na Axel anaolea na mwenza wake aitwae Daniel Yona Jr.[2]

Elimu[hariri | hariri chanzo]

Mwanaharakati huyu alisoma shule ya msingi Bunge iliyopo jijini Dar-es-salaam. Na kuendelea na elimu yake ya sekondari katika shule ya Forodhani na Mkwawa. Irene alichaguliwa kuendelea na elimu ya juu katika Chuo Kikuu Cha Dar-es-salaam na kupata Shahada yake ya kwanza ya Mahusiano ya Kimataifa na Utawala wa Umma. Baadae alipata Shahada yake ya uzamili katika masomo ya Utawala wa Biashara mnamo mwaka 2011.[3]

Harakati[hariri | hariri chanzo]

Licha ya kuwa na ujuzi wa takribani miaka kumi katika vyombo vya habari kama mtangazaji na mtayarishaji vipindi "East Africa Television" na "IPP Media",Irene Kiwia amekuwa na mchango mkubwa katika maendeleo ya jamii nchini Tanzania na barani Afrika kwa ujumla. Mnamo mwaka 2009 alianzisha "NGO" itwayo Tanzania Women of Achievement ili kuwawezesha wanawake kuwa na nafasi kuchangia katika maswala ya jamii,siasa,uchumi na utamaduni nchini.[4] Mnamo mwaka 2010 alishiriki katika "Fortune/US State Department Women Mentoring Program".Irene pia alihudhuria katika mkutano mkubwa wa "UN General Assembly Health and Young Girl’s Empowerment Forums" kama mtu wa diplomasia mnamo mwaka 2014. Katika mwaka 2015 alikuwa mwanamke wa mwaka wa tuzo za "Africa Reconnect" kwa mchango wake wa kuwezesha wanawake katika mambo mbalimbali ya kijamii,siasa,uchumi na utamaduni barani Afrika.[5]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-09-17. Iliwekwa mnamo 2018-10-20.
  2. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-09-17. Iliwekwa mnamo 2018-10-20.
  3. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-09-17. Iliwekwa mnamo 2018-10-20.
  4. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-10-05. Iliwekwa mnamo 2018-10-20.
  5. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-09-17. Iliwekwa mnamo 2018-10-20.