Ida Mntwana

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ida Fiyo Mntwana

Amekufa 1960(umri 57)
Nchi Afrika Kusini
Majina mengine Ida Mntwana
Kazi yake Mshonaji mavazi na Mwanasiasa


Ida Mntwana alifanya kazi kama mshonaji mavazi akajishughulisha na siasa katika miaka ya 1950. [1] Baada ya Madie Hall Xuma kujiuzulu kama rais wa kitaifa wa Umoja wa Wanawake wa African National Congress (ANCWL) mwaka wa 1949, Mntwana alikuwa mbadala wake. Mntwana alikuwa mkali zaidi kuliko mtangulizi wake, akipanga wanawake katika maandamano, migomo na vitendo vingine vya uasi wa raia . [2] Pia alichaguliwa kuwa mmoja wa kamati kuu ya ANC (Africa National Congress ) [3]

Mnamo 1954, Mntwana alikuwa rais wa kwanza wa Shirikisho la Wanawake wa Afrika Kusini (FEDSAW). Alisaidia kuandaa Kongamano la Wananchi. [4] Siku ya pili ya kongamano hilo, polisi walivamia mkutano huo na kuzua mzozo kati ya wananchi na polisi. Ni Mntwana aliyetuliza wananchi kwa kuimba wimbo wa uhuru akiwa jukwaani ili kongamano liendelee vizuri. [5]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "60 Iconic Women — The people behind the 1956 Women's March to Pretoria (21–30)". 
  2. Khaminwa, Muhonjia (2002). "Mntwana, Ida (fl. 1949–1955)". Women in World History: A Biographical Encyclopedia. Gale Research Inc. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-09-21 – kutoka HighBeam Research.  Unknown parameter |url-access= ignored (help)
  3. "Ida Fiyo Mntwana". South African History Online. 27 August 2011. Iliwekwa mnamo 13 September 2016.  Check date values in: |date=, |accessdate= (help)
  4. "Ida Fiyo Mntwana". South African History Online. 27 August 2011. Iliwekwa mnamo 13 September 2016.  Check date values in: |date=, |accessdate= (help)
  5. "Congress of the People - I was there | South African History Online". www.sahistory.org.za. 1 September 2019. Iliwekwa mnamo 2020-07-14.  Check date values in: |date= (help)