Hukwe Zawose

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Hukwe Zawose mnamo mwaka 2003 kwenye Jubilee Diamnond Hall, Dar es Salaam(picha:Issa Michuzi)
Wanawe Hukwe Zawose wanaendeleza muziki yake (picha:Issa Michuzi)

Hukwe Zawose ((* 1940 Bugiri - † 30 Desemba 2003 Bagamoyo) huyu alikuwa ni mwanamuziki wa kiasili wa kitanzania, na muziki wake hasa ulikuwa ni wa kabila la Wagogo. Ala aliyotumia zaidi ilikuwa ilimbal pamoja na zeze; alipiga pia filimbi.

Kipaji chake cha muziki kiligunduliwa na aliyekuwa rais wa kwanza wa Tanzania hayati J. K. Nyerere wakati alipofanya ziara mkoa wa Dodoma. Alivutiwa na muziki wa Hukwe, na aliporudi Daressalaam alimuita Hukwe kwenye kikundi cha utamaduni cha Taifa Bagamoyo Players.

Katika miaka ya 1990 Zawose alirekodi muziki pamoja na Peter Gabriel na kutoa CD kadhaa.

Albamu Kadhaa[hariri | hariri chanzo]