Gertrude Mwangala

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Gertrude Mwangala Akapelwa (alizaliwa Zambia, 1948[1]) ni mhandisi wa zamani wa mifumo ya IBM wa Zambia na Meneja wa zamani wa Idara ya Miundombinu na Uendeshaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika ICT,ambaye anahudumu kama Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Teknolojia cha Victoria Falls (VFU), taasisi ambayo alisaidia katika uanzishaji wake mwaka wa 2002. [2]

Maisha na elimu[hariri | hariri chanzo]

Alijiunga na Chuo Kikuu cha Zambia mnamo 1969, na kuhitimu masomo  yake 1973 na kutunukiwa Shahada ya Sayansi katika Hisabati na Elimu.Shahada yake ya Uzamili ya Utawala wa Umma, aliyobobea katika Sera na Usimamizi wa Umma, alisoma katika chuo cha  Harvard University's Kennedy School of Government, mwaka 1997. Pia amepata tasnifu yake ya shahada ya Udaktari wa Elimu kupitia utafiti aliyotunukiwa na Chuo Kikuu cha Liverpool mwaka wa 2018. Udaktari wake ni kuhusu Elimu ya Juu na Utawala wa Elimu ya Juu.[3]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Zambia National Commercial Bank PLC (ZMBAY.PK) People | Reuters.com". web.archive.org. 2017-11-23. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-11-23. Iliwekwa mnamo 2022-03-16. 
  2. "School of Education". liberalarts.vt.edu (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2022-03-16. 
  3. Akapelwa-Ehueni, Gertrude Mwangala (15 November 2017). "Gertrude Mwangala Akapelwa-Ehueni: Chairperson of the Board at Zambia Information and Communications Technology Authority (ZICTA)". LinkedIn. Iliwekwa mnamo 15 November 2017.  Check date values in: |date=, |accessdate= (help)