Gari la Nyayo
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Gari la Nyayo ilikuwa mradi wa serikali ya Kenya wa kupanga na kutengeneza magari ya Kenya. Mradi huu ulianzishwa 1986 wakati kisha rais, Daniel arap Moi aliuliza Chuo Kikuu cha Nairobi kutengeneza magari.
Majaribio matano yalifanywa yaitwayo Pioneer Nyayo Cars na yalikuwa na kasi ya 120 km/h. Shirika la magari la Nyayo liliundwa ili kuzalisha magari haya kwa wingi. Hata hivyo, kutokana na ukosefu wa fedha, magari haya hayakuingizwa katika uzalishaji.
Shirika la magari la Nyayo baadayelilipewa jina la Numerical Machining Complex Limited , shirika la kuunda viungo vya chuma vya viwanda vingine.