Nenda kwa yaliyomo

Wanyama wa nyumbani

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Faida za mifugo)
Ng'ombe machungani.
Ng'ombe aina ya Żubroń.
Mifugo ya nyumbani

Wanyama wa nyumbani au wanyama-kaya au mifugo (kutoka kitenzi "kufuga") ni wale wanyama ambao huishi katika mazingira ambayo mwanadamu anaishi na hawawezi kumuathiri kwa kiasi kikubwa. Wanyama hao wanatunzwa kwa uangalizi wa binadamu kwa ajili ya ulinzi, michezo, kazi, pambo na majaribio ya maabara.

Tangu milenia kadhaa wanyama hao wamepatana na wanadamu, nao ni kama vile mbwa, mbuzi, nguruwe, kondoo, ng'ombe, paka, kuku, punda, bata, nyuki, ngamia, farasi, njiwa, kware na wengine wengi.

Wanyama hao wana faida katika maisha ya wanadamu; kwa mfano:

  • ng'ombe hupatia watu maziwa, nyama, pia ngozi yake inaweza kutumika kutengeneea vitu mbalimbali.
  • mbwa husaidia hasa katika suala la ulinzi katika mazingira yanayomzunguka mwanadamu.
  • mbuzi huwapatia watu nyama, maziwa ila si mazuri kama yale ya ng'ombe na pia ngozi yake hutumika kutengenezea vitu kama vile ngoma, hasa katika jamii za Afrika.
  • kware ni ndege mdogo; mayai yake ni madogo sana yana faida kubwa katika mwili wa mwanadamu kwa sababu yanasemekena kutibu baadhi ya magonjwa katika miili yetu.

Mifugo hii huwa na faida nyingi sana kwa mwanadamu, kwa hiyo anashauriwa kuwafuga kwa ajili ya faida zifuatazo:

  • 1. Mifugo kama vile ng'ombe na mbuzi hutupatia maziwa ambayo hutusaidia kupata protini ambayo husaidia mwili kukua na pia huulinda mwili dhidi ya magonjwa.
  • 2. Mifugo pia hutupatia nyama, ambayo hutupata protini ambayo husaidia mwili kukua na pia kulinda mwili dhidi ya magonjwa.
  • 3. Mifugo hutupatia pesa kwa kuuza nyama, maziwa, ngozi, kwato, mbolea na hata wanyama wenyewe.
  • 4. Ngozi ya mifugo hutumika kutengenezea vitu kama vile ngoma, viatu, mikanda, nguo. Vitu vinavyotengenezwa kwa kutumia ngozi ni imara na pia hudumu kwa muda mrefu.
  • 5. Kwato za wanyama hawa hutumika kutengenezea vyombo kama sahani,vibakuli, na kadhalika.
  • 6. Mavi ya wanyama hutumika kama mbolea ambayo huwezesha mazao kukua haraka na kustawi vizuri.
  • 7. Wanyama pia hutumika kwa tiba. Wagonjwa wanaohitaji wanyama katika matibabu yao hupewa ruhusa maalum kusafiri na kuishi na wanyama hata sehemu ambazo wanyama hawakubaliwi.

Wanyama wana faida nyingi sana; hizi ni chache tu. Wanyama hao hutoa pia faida za kihisia kama mazoezi, mahusiano ya kijamii na n.k. Wanyama hawa huondoa upweke kwa watu wasiokuwa na marafiki au mahusiano ya kijamii kama wazee, watoto, wajawazito. Wanyama wengine huwatembelea wagonjwa.

Wanyama hawa hufundiswa jinsi ya kufanya vitu vya kisayansi, kwa kulenga wagonjwa.

Hivyo tunaweza kuona faida za wanyama hao: inafaa tuwatunze vizuri kwani tunawategemea katika shughuli mbalimbali za kijamii na za kiuchumi. Hivyo hawatakiwi kupigwa ovyo. Wanatakiwa waangaliwe afya zao na kupata mahitaji yao.

Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Wanyama wa nyumbani kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.