Dennis Brutus
Dennis Brutus (28 Novemba 1924 - 26 Desemba 2009) alikuwa mwandishi wa Afrika Kusini. Kwa vile aliandika dhidi ya ubaguzi wa rangi alifungwa jela na baadaye kuishi uhamishoni 1966-1990.[1] Hasa alitunga mashairi na alifundisha kama profesa wa ushairi nchini Marekani.
Wasifu
[hariri | hariri chanzo]Dennis Brutus alizaliwa tarehe 28 Novemba, mwaka wa 1924 mjini Salisbury, Rhodesia, ambapo sasa huitwa Harare nchini Zimbabwe. Alisoma kwenye Paterson High School nchini Afrika Kusini na kupata shahada yake ya kwanza kutoka Chuo Kikuu cha Fort Hare katika somo la Kiingereza mwaka wa 1947. Mwaka wa 1950 alimwoa May Jaggers, wakawa na watoto wanane. Kuanzia 1948 hadi 1961, Brutus alifundisha Kiingereza na Kiafrikaans kama mwalimu wa sekondari mjini Port Elizabeth. Mwaka wa 1960 alianza pia kufanya kazi kama mwandishi wa habari. Kwa vile aliandika dhidi ya siasa ya apartheid, alifungwa jela kisiwani mwa Robben kwa miezi 18 (1964-65), na kutoka Afrika Kusini mwaka wa 1966. Uhamishoni kwanza alifanya kazi mjini London kwa shirika la International Defence and Aid Fund. Mwaka wa 1971 akahamia Marekani. Kule akawa profesa wa chuoni, kwanza kwa somo la Kiingereza katika Chuo Kikuu cha Northwestern mjini Evanston (1971-85), na hatimaye tangu mwaka wa 1986 akawa profesa katika idara ya elimu ya kijamii ya watu weusi, Chuo Kikuu cha Pittsburgh.
Maandishi yake [2][3]
[hariri | hariri chanzo]- Sirens, Knuckles, Boots (mashairi, 1963)
- Letters to Martha (mashairi, 1968)
- Poems from Algiers (mashairi, 1970)
- Thoughts Abroad (mashairi, 1970, aliyoyatolea chini ya jina la John Bruins)
- A Simple Lust (mashairi, 1973)
- China Poems (mashairi, 1975)
- Stubborn Hope (mashairi, 1978)
- Salutes and Censures (mashairi, 1982)
- Airs and Tributes (mashairi, 1989)
- Still the Sirens (mashairi, 1993)
- Remembering Soweto (mashairi, 2004)
- Leafdrift (mashairi, 2005)
Angalia pia
[hariri | hariri chanzo]Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Ukurasa 484 wa Chapman, Michael. 2003. Southern African Literatures, University of Natal Press. ISBN 1-86914-028-1
- ↑ Chapman, Michael. "Dennis Brutus: 1924-2009.(Obituary)." Current Writing: Text and Reception in Southern Africa. Program of English Studies, University of Natal. 2010. Imeangaliwa tarehe 16 Aprili 2012 kupitia HighBeam Research Ilihifadhiwa 31 Machi 2002 kwenye Wayback Machine. (lazima kusajiliwa).
- ↑ "AFRICA ACTION grieves death of Dennis Vincent Brutus, 1924-2009." States News Service. 2009. Imeangaliwa tarehe 16 Aprili 2012 kupitia HighBeam Research Ilihifadhiwa 31 Machi 2002 kwenye Wayback Machine. (lazima kusajiliwa).