Danny Drinkwater

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Danny Drinkwater.

Daniel Noel Drinkwater (amezaliwa 5 Machi 1990) ni Mwingereza ambaye ni mchezaji wa mpira wa miguu na ambaye anacheza kama kiungo kwenye klabu ya Chelsea na timu ya taifa ya Uingereza.

Yeye awali alicheza kwa mkopo katika timu za Huddersfield Town, Cardiff City, Watford na Barnsley, na pia aliitumikia Manchester United na Leicester City.

Drinkwater alicheza kimataifa kwenye timu ya taifa ya Uingereza ngazi ya chini ya miaka 18 na chini ya miaka 19. Akiwa Leicester City walishinda kombe la Ligi Kuu ya Uingereza msimu wa 2015 – 16.

Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Danny Drinkwater kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.