CHAKICHUKIDA

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

CHAKICHUKIDA au siku hizi CHAWAKAMA-UDSM (kirefu chake: Chama cha Kiswahili cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam) ni jina la chama cha Kiswahili cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.[1][2] Chama kilianzishwa mnamo mwaka wa 1972 na wanafunzi wa mwanzo kabisa walioingia Chuo Kikuu ili kusomea Kiswahili katika ngazi ya shahada.[3]

Chama hiki kilikuwa na madhumuni makuu mawili:

  1. Dhumuni la kwanza lilikuwa kuwapa wanafunzi nafasu ya kuvumbua na kukuza vipawa vyao katika isimu na fasihi ya Kiswahili.
  2. Dhumu la pili lilikuwa kuamsha ari ya mapinduzi ya kuendeleza matumizi ya lugha ya Kiswahili kwa njia ya uchunguzi zaidi wa kimaandishi.

Kama ilivyo vyama na taasisi nyingine za miaka ya awali zilizokuwa zikijishughulisha na kazi ya uenezi wa Kiswahili, hii nayo iliweza kupata mafanikio yake nayo ni:

  • (a) Baada ya kuanzishwa, chama hiki kiliweza kutoa jarida ambalo lilijulikana kama Kiswahili, fasihi na ufanisi toleo la kwanza ambalo baadaye lilibadilishwa jina na kuitwa Kioo cha Lugha. Hivi sasa jarida hilo linaitwa "Mulika".
  • (b) Chama kimeweza pia kutoa nafasi kwa walimu, wanafunzi na wadau wengine wa lugha ya Kiswahili kujadili na kuhakiki fani mbalimbali za fasihi na simu kupitia jarida lake.
  • (c) Hali kadhalika chama kimeweza kutoa jarida linaloitwa Zinduko, ambalo makala yake hutoka kwa wahadhiri wa lugha ya Kiswahili.
  • (d) Chama pia kimeweza kuendesha makongamano mbalimbali kuhusu fani za fasihi na isimu ya Kiswahili.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Mahenge, Elizabeth Godwin (2015-09-24). Kiswahili kwa wageni: Kiongozi cha mwalimu (kwa Kiswahili). Dl2a - Buluu Publishing. ISBN 9791092789 Check |isbn= value (help). 
  2. "CHAWAKAMA-UDSM: Kuhusu Sisi". CHAWAKAMA-UDSM. Iliwekwa mnamo 2018-09-02. 
  3. "EDUCATION". hamimam.blogspot.com (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2018-09-02.