Burj Dubai

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Burj Dubai wakati 2008

Burj Dubai (Kiarabu برج دبي‎ - Mnara wa Dubai) ni jengo kubwa la maghorofa linaloendelea kujengwa nchini Dubai (Falme za Kiarabu) tangu mwaka 2004. Litakapokamilika mwaka 2009 litakuwa jengo lenye kimo kikubwa duniani.

Burj Dubai inatarajiwa kufungulia Septemba 2009. Mipango kamili bado ni siri lwa sababu wajenzi wanataka kuwa na uhakika ya kwmaba itakuwa jengo kubwa duniani. Hivyo wameandaa kuongeza ghorofa kama jengo lingine linaendelea kujengwa popote duniani. Kwa sasa inasemekana kuwa na ghorofa 162 na eneo la vyumba vyote ni 334,000 m². Ghorofa ya juu itaishia kwa mita 643 na antenna juu yake itafikia mita 818. Gharama zilipangwa kuwa bilioni za dolari 14.1.

Ghorofa 37 za kwanza zitakuwa hoteli. Juu yake kuna makazi 779 katika ghorofa 38-108 na 700 yameshauzwa. Ghorofa za juu zitakuwa na ofisi na makazi maalumu.

[hariri] Picha za ujenzi

WikiLettreMini.svg Makala hiyo kuhusu "Burj Dubai" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri".

Ikiwepo makala kuhusu Burj Dubai kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili.