Bugembe

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ramani ya Uganda
Majira nukta kuonesha mji wa Bugembe 0°28'03.0"N, 33°14'29.0"E

Bugembe ni mji katika wilaya ya Jinja uliopo eneo la mashariki mwa Uganda. Ndipo ulipo utawala wa kifalme wa Busoga, moja kati falme nne halali kikatiba nchini Uganda, ambao inapakana na mkoa mdogo wa Busoga.

Mahali[hariri | hariri chanzo]

Bugembe inakadiriwa kuwepo umbali wa kilomita 8, kwa barabara, katika wilaya ya Jinja, ndio mji mkubwa katika eneo hilo la mkoa mdogo.[1] Mji huu upo kwenye barabara kuu katikati ya miji ya Jinja na Iganga. Majira nukta ya Bugembe ni:0°28'03.0"N, 33°14'29.0"E (Latitudo:0.467500; Longitudo:33.241389). Mji huu upo katika mwinuko wa wastani wa mita 1269 kutoka usawa wa bahari.[2]

Idadi ya watu[hariri | hariri chanzo]

Mwaka 2002, sensa ya taifa ilitoa idadi ya watu kwenye mji huo kuwa ni 26,268. mwaka 2010, Ofisi ya takwimu ya Uganda ilikadiria idadi ya watu kuwa ni 32,200. Mwaka 2011, Ofisi ya takwimu ilikadiria idadi ya watu katikati ya mwaka kuwa ni 33,100.[3]

Maeneo muhimu[hariri | hariri chanzo]

Yafuatayo ni maeneo muhimu yaliyopo kwenye mipaka ya mji ama yanayozunguka mji:

  • Ofisi ya halmashauri ya mji wa Bugembe
  • Makao makuu ya ufalme wa Busoga
  • Makazi ya askari polisi wa Uganda
  • Shule ya msingi Nakanyangi.
  • Shule ya msingi Jinja Lake View
  • Shule ya sekondari ya wasichana ya Nakanyonyi
  • Shule ya Sekondari ya St. Thaddeus
  • Soko kuu la Bugembe
  • Kituo cha afya cha Bugembe
  • Shule ya sekondari ya St. Florence
  • Shule ya sekondari ya Vic View (Vic View High School)
  • Shule ya sekondari ya wasichana ya Wanyange

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Road Distance Between Jinja and Bugembe With Map". Globefeed.com. Iliwekwa mnamo 3 July 2015.  Check date values in: |accessdate= (help)
  2. FMN, . (3 July 2015). "Elevation of Bugembe, Uganda Elevation Map, Topo, Contour". Floodmap.net (FMN). Iliwekwa mnamo 3 July 2015.  Check date values in: |date=, |accessdate= (help)
  3. "Estimated Population of Bugembe In 2002, 2010 & 2011" (PDF). Uganda Bureau of Statistics. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 7 July 2014. Iliwekwa mnamo 3 July 2015.  Unknown parameter |url-status= ignored (help); Check date values in: |archivedate=, |accessdate= (help)