Brangelina

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Pitt na Jolie kwenye sherehe ya 81st Academy Awards mnamo Februari 2009

Brangelina ni jina linalojumuisha muigizaji Brad Pitt wa kutoka Marekani aliyeigiza katika filamu zaidi ya 40 (kama Fight Club, Se7en, Mr. & Mrs. Smith) na Angelina Jolie ambaye ni balozi wa shirika la Umoja wa Mataifa na vilevile muigizaji wa filamu kama Lara Croft: Tomb Raider na Changeling.

Yaliyomo

[hariri] Historia

[hariri] Brad Pitt

Katika miaka ya nyuma, Pitt amewahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na waigizaji wengi kama Robin Givens, Jill Schoelen, na Juliette Lewis.[1] Pitt pia alikuwa mchumba wake Gwyneth Paltrow, aliyekuwa na uhusiano naye kuanzia mwaka wa 1995 hadi 1997.[2]

Pitt alionana na muigizaji wa kipindi cha Friends aitwaye Jennifer Aniston mnamo 1998 na wakaoana mjini Malibu mnamo Julai 29, 2000.[3] Mnamo Januari 2005, Pitt na Aniston walitangaza kuwa wameachana baada ya kuoana kwa muda ya miaka saba.[4]

[hariri] Angelina Jolie

Makala kuu ya: Angelina Jolie

Mnamo Machi 28, 1996, Jolie aliolewa na muigizaji Muingereza Jonny Lee Miller.[5] Jolie na Miller waliachana mwaka uliofuata na talaka ikatolewa mnamo Februari 3, 1999. Mnamo Mei 5, 2000, aliolewa na muigizaji wa Marekani anayeitwa Billy Bob Thornton, na wakawachana mnamo Mei 27, 2003.

[hariri] Uhusiano wao

Jolie na Pitt kwenye Deauville American Film Festival mnamo Septemba 2007.

Jolie na Pitt walikutana walipokuwa wanaigiza katika filamu ya Mr. & Mrs. Smith na uhusiano wao ulijulikana sana kwenye Hollywood .[6]. Inasemekana kuwa Pitt na Jolie walipendana pindi Pitt bado alikuwa na Jennifer Aniston, lakini wote wamekataa madai haya; wakisema kuwa walipendana walipukuwa wakiigiza filamu hii.[7] Uhusiano wa Pitt na Jolie ulithibitishwa wakati picha zilitoka za kuonyesha Pitt akiwa na Jolie na mwanawe Maddox kwenye bahari nchini Kenya.[8] Wawili hawa walionekana wakiwa pamoja mara nyingi, na watangazaji wakawabandika wapenzi hawa jina la "Brangelina".[9] Mnamo Januari 11, 2006, Jolie alitangaza kuwa alikuwa na mimba ya Brad Pitt.[10]

[hariri] Watoto

[hariri] Marejeo

  1. Brad Pitt. People. Rudishwa juu ya March 12, 2008.
  2. Gliatto, Tom. "Love Lost", June 30, 1997. 
  3. Brad Pitt Biography. People. Rudishwa juu ya May 16, 2008.
  4. "Pitt and Aniston announce split", BBC News, BBC, January 8, 2005. Retrieved on 2009-03-19. 
  5. * Bandon, Alexandra. Following, Ambivalently, in Mom or Dad's Footsteps. The New York Times. August 25, 1996. Accessed February 25, 2009.
  6. Silverman, Stephen M.. "How Will Brad and Angelina's Movie Fare?", People, January 21, 2005. Retrieved on March 16, 2009. 
  7. Harris, Mark. The Mommy Track. The New York Times. October 15, 2008. Accessed October 18, 2008.
  8. Brad & Angelina's Latest Getaway. People (May 4, 2005). Rudishwa juu ya May 16, 2008.
  9. Newcomb, Peter. "Angelina Jolie, Brad Pitt", Vanity Fair, September 2, 2008. Retrieved on April 3, 2009. 
  10. Angelina Jolie Pregnant. People (January 11, 2006). Rudishwa juu ya May 15, 2008.
Vifaa binafsi
Maeneo ya wiki

Vibadala
Vitendo
Urambazaji
Vifaa
Lugha zingine