Bonnah Kaluwa
Bonnah Moses Kaluwa (amezaliwa 29 Disemba, 1978) ni mwanasiasa, mwanaharakati na mbunge wa jimbo la Segerea kupitia Chama cha Mapinduzi akiwawakilisha wananchi wa jimbo hilo tangu Novemba 2015, alipochaguliwa kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huo.
Kabla ya kuwa mbunge, Bonnah alikuwa Diwani wa kata ya Kipawa kwa miaka mitano kuanzia mwaka 2010.
Elimu yake
[hariri | hariri chanzo]Bonnah alipata elimu yake ya msingi katika shule ya msingi Kalangala kuanzia 1985 na kuhitimu 1991. Na akaendelea na elimu ya sekondari katika shule ya sekondari Mwenge kuanzia 1992 na kuhitimu 1996. Akajiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kitengo cha Computer (UCC) na kuhitimu ngazi ya cheti kwenye Business Information and Technology (CBIT) mwaka 2007. Mwaka 2012' alihitimu shahada ya IT and Business Management (BSc IT & BM) kutoka College Learn IT. Akajiunga Centre of Foreign Relations, alihitimu na kutunukiwa Post Graduate Diploma in Management and Foreign Relations ambapo tafiti aliyofanya ilihusu Madhara ya uhamiaji haramu kwenye usalama wa binadamu
Siasa
[hariri | hariri chanzo]Bonnah alianza mapema sana kujihusisha na mambo ya siasa ambapo alikuwa mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi kwa muda mrefu. Baada ya kuguswa sana na matatizo yaliyokuwa yakiwakabilli wakazi wa Kipawa, Bonnah aliamua kugombea nafasi ya Udiwani kata ya Kipawa na kushinda.[1]
Harakati na Miradi ya Maendeleo
[hariri | hariri chanzo]Wamama na maendeleo
[hariri | hariri chanzo]Akiwa Diwani, Bonna alianzisha Wamama na Maendeleo (WANAMA) iliyoendesha semina ya ujasiriamali kwa wakinamama wa Kipawa takriban 500. Kupitia mradi huu, wakinamama hawa walifanikiwa kupata mikopo midogo midogo kwa ajili ya kuendesha biashara zao kupitia vikundi.
Mazingira bora kwa elimu bora
[hariri | hariri chanzo]Mradi huu ulianzishwa baada ya Bonnah kuguswa na mazingira mabaya na hatarishi kwa wanafunzi na walimu wa kata ya Kipawa. Mafanikio yaliyopatikana kupitia mradi huu ni pamoja na: Kuboresha miundombinu na mazingira ya shule, Kujenga shule 7 kwenye kata, Kuongeza madara kwenye shule zilizokuwa na upungufu wa madarasa, Kuchangia madawati katika shule za sekondari, msingi na za awali, Kuchimba visima vya maji safi na salama kwenye shule 2 za sekondari na 3 za msingi.
Elimu mwanzo mwisho
[hariri | hariri chanzo]Kampeni hii iliendeshwa kupitia ufadhili wa kampuni ya Tigo ambapo ulijikita katika kuhamasisha kujiendeleza kupitia mashindano ya mitindo ya mitaani (Street fashion show). Takriban USD 20,000 zilikusanywa kwenye harambee.
Ujenzi wa zahanati
[hariri | hariri chanzo]Kwa mara ya kwanza tangu Uhuru kata ya Kipawa imeweza kujenga zahanati na kuondoa tatizo la kusafiri umbali mrefu kupata huduma ya matibabu.
Bonnah Education Trust Fund
[hariri | hariri chanzo]Mfuko wa elimu wa Bonnah Kaluwa ulianzishwa mwaka 2012 lengo kuu likiwa ni kuhakikisha watoto wenye mahitaji maalum wanapata elimu. Tangu kuanzishwa kwa mfuko huu, zaidi ya wanafunzi 100 kwa mwaka wamefanikiwa kupata elimu.[2]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Wasifu wa Bonnah". 22 Novemba 2015. Iliwekwa mnamo 21 Disemba 2016.
{{cite web}}
: Check date values in:|accessdate=
(help) - ↑ "Harakati za Bonnah". 11 Febuari 2016. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-08-25. Iliwekwa mnamo 21 Disemba 2016.
{{cite web}}
: Check date values in:|accessdate=
na|date=
(help)