Bob Marley & The Wailers
Bob Marley & The Wailers | |
---|---|
| |
Maelezo ya awali | |
Asili yake | Kingston, Jamaica |
Aina ya muziki | Reggae, ska, rocksteady, roots reggae |
Miaka ya kazi | 1963–1981 |
Studio | Island, Tuff Gong, Trojan, Studio One, Beverley's |
Ame/Wameshirikiana na | The Wailers Band, The Original Wailers, The Upsetters, I Threes |
Wanachama wa zamani | |
Bob Marley Peter Tosh Bunny Wailer Cherry Smith Beverley Kelso Junior Braithwaite Constantine Walker Hugh Malcolm Aston Barrett Carlton Barrett Earl Lindo Alvin Patterson Rita Marley Marcia Griffiths Judy Mowatt Al Anderson Tyrone Downie Junior Marvin |
Bob Marley & The Wailers lilikuwa kundi la muziki wa reggae kutoka nchini Jamaika. Bendi ilianzishwa na Bob Marley. Kundi liliundwa wakati mwanamuziki aliyejifunza mwenye Hubert Winston McIntosh (Peter Tosh) alivyokutana na Neville Livingston (Bunny Wailer), na Robert Nesta Marley (Bob Marley) mnamo mwaka wa 1963 na kuwafunza namna ya kupiga gitaa, vinanda, na tumba.
Mwishoni mwa miaka ya 1963 Junior Braithwaite, Beverley Kelso, na Cherry Smith wakajiunga na The Wailers. Baada ya Peter Tosh na Bunny Wailer kuondoka katika bendi mnamo 1974, Bob Marley akaanza kufanya ziara na wanachama wapya wa bendi. Waitikiaji wake wapya walikuwa ni pamoja na kina ndugu Carlton na Aston "Family Man" Barrett katika upande wa magoma na besi kwa ujumla, Junior Marvin na Al Anderson walipiga gitaa, Tyrone Downie na Earl "Wya" Lindo upande wa vinanda, na Alvin "Seeco" Patterson katika upande wa tumba. Kina "I Threes", ikiunganishwa na Judy Mowatt, Marcia Griffiths, na mke wa Marley, Rita, walisaidia upande wa sauti za uitikiaji kwa nyuma.
Historia
[hariri | hariri chanzo]Kundi liliundwa wakati mwanamuziki aliyejifunza mwenye Hubert Winston McIntosh (Peter Tosh) alivyokutana na Neville Livingston (Bunny Wailer), na Robert Nesta Marley (Bob Marley) mnamo mwaka wa 1963 na kuwafunza namna ya kupiga gitaa, vinanda, na tumba.
Awali walifahamika kwa majina tofauti-tofauti kama vile The Teenagers, The Wailing Rudeboys, The Wailing Wailers mwisho kabisa The Wailers. Mwaka wa 1966 Braithwaite, Kelso na Smith wakaondoka katika bendi, ambapo wakabaki mtu tatu Livingston, Marley na Tosh (Neville Livingston huwa jina la kuzaliwa la Bunny Wailer).
Miongoni mwa nyimbo kali za The Wailers zilirekodiwa na Lee "Scratch" Perry na bendi yake ya studio The Upsetters. Mwanzoni mwa miaka ya 1970 wanachama wa The Upsetters Aston "Family Man" Barrett na kaka'ke Carlton (Carlie) Barrett,[1] wakaanzisha Wailers Band, wanatoa ala tupu za kusaidia The Wailers. The Wailers wamepata kurekodi kazi kadhaa za reggae na ska kama vile "Simmer Down", "Trenchtown Rock", "Nice Time", "War", "Stir It Up" na "Get Up, Stand Up".
The Wailers waliachana mnamo mwaka wa 1974 baada ya Tosh na Livingston kukataa kufanya ziara ya muziki. Bob Marley akaanzisha Bob Marley & The Wailers akiwa yeye mwenyewe mpiga gitaa, mtunzi wa nyimbo na mwimbaji mkuu, kundi la Wailers Band wakiwa kama wasaidizi, na kina I Threes wakiwa kama waitikiaji. The Wailers Band wakiwa pamoja na kina Carlton Barrett na "Family Man" Barrett katika upande wa ngoma na besi, Junior Marvin na Al Anderson wakipiga solo gitaa, Tyrone Downie na Earl "Wya" Lindo wanapiga kinanda, na Alvin "Seeco" Patterson anapiga tumba. The I Threes inaunganishwa na mke wa Bob Marley Rita Marley, Judy Mowatt na Marcia Griffiths.
Wanachama
[hariri | hariri chanzo]- Bob Marley & The Wailers timeline
Diskografia
[hariri | hariri chanzo]- The Wailing Wailers (1965)
- Soul Rebels (1970)
- Soul Revolution (1971)
- The Best of The Wailers (1971)
- Catch a Fire (1973)
- Burnin' (1973)
- Natty Dread (1974)
- Rastaman Vibration (1976)
- Exodus (1977)
- Kaya (1978)
- Survival (1979)
- Uprising (1980)
- Confrontation (1983)
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Lee Scratch Perry Interview, New Musical Express, 17 Novemba 1984
Soma zaidi
[hariri | hariri chanzo]- Masouri, John (2007) Wailing Blues: The Story of Bob Marley's "Wailers" Wise Publications ISBN 1-84609-689-8
- Farley, Christopher (2007). Before the Legend: The Rise of Bob Marley, Amistad Press ISBN 0-06-053992-5
- Goldman, Vivien (2007) The Book of Exodus: The Making and Meaning of Bob Marley and the Wailers' Album of the Century Three Rivers Press ISBN 1-4000-5286-6
- Colin Grant (2011) The Natural Mystics : Marley, Tosh, Wailer, Jonathan Cape 978-0-224-08608-0 (U.K.), W.W. Norton & Company ISBN 978-0-393-08117-6 (U.S.)
Viungo vya Nje
[hariri | hariri chanzo]- Official website
- Bob Marley Guitar Lessons Ilihifadhiwa 31 Mei 2013 kwenye Wayback Machine.