Beth Mugo
Beth Wambui Mugo (amezaliwa tar. 11 Julai 1939) ni mwanasiasa na mwanabiashara nchini Kenya. Anatoka katika familia ya Mzee Jomo Kenyatta akiwa binamu wa Uhuru Kenyatta. 2007 alirudi kama mbunge wa Dagoretti (Nairobi) kwa jina la chama cha PNU.
Mugo alisoma Marekani akawa mwalimu mkuu wa Shule ya Msingi wa Kiganjo akaendelea kufanya kazi na Voice of Kenya akashughulika biashara mbalimbali. 1992 alikuwa kati ya waanzilishaji wa chama cha DP.
1997 alijiunga na SDP akaingia bungeni kwa jimbo la Dagoretti. Katika uchaguzi wa 2002 aligombea upande wa maungano ya NARC ambamo chama cha SDP ilikuwa mshiriki akarudishwa.
Katika serikali ya kwanza ya Mwai Kibaki alikuwa waziri mdogo katika wizara ya elimu akiangalia hasa elimu ya msingi na programu ya NARC ya kuondoa karo ya shule kwenye ngazi hii.
Wakati wa kuporomoka kwa NARC baada ya kura maalumu ya wananchi juu ya katiba ya 2005 alikuwa kati ya wanasiasa upande wa rais Kibaki waliojaribu kujenga NARC-Kenya akawa mwenyekiti wa chama hiki kwa muda.
Kabla ya uchaguzi wa 2007 alijiunga na PNU.
Viungo vya Nje
[hariri | hariri chanzo]- Ukurasa wa serikali wa kumtambulisha Beth Mugo Ilihifadhiwa 22 Novemba 2007 kwenye Wayback Machine.