Nenda kwa yaliyomo

Athi River Mining

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Athi River Mining (kifupi ARM) ni kampuni ya kibiashara nchini Kenya inayochimba madini na kutengeneza bidhaa kama saruji, mbolea wa kilimo, aina kadhaa za chokaa na minerali mingine kwa matumizi ya viwandani na katika ujenzi.

Kampuni ilianzishwa na Bwana H.J. Paunrana mwaka 1975 mjini Athi River na makao makuu yake yapo Nairobi. Kiasili iliana kuchimba mawe ya chokaa katia eneo la Athi River na kuusafisha, kusaga na kuuza.

ARM ina migodi na viwanda katika Kenya, Tanzania na Afrika Kusini.

  • Saruji yake inayouzwa chini ya jina la "Rhino" hutengenezwa huko Kaloleni, Mombasa.
  • Silikati ya sodiamu hutengenezwa Athi River na Afrika Kusini.
  • Chokaa safi kwa matumizi ya viwandani (karatasi) na ujenzi wa barabara hutengenezwa Athi River, Kaloleni na Tanga.
  • Mbolea wa kilimo unatengenzwa Athi River vilevile na kuuzwa kwa jina la "Mavuno"
  • Minerali mbalimbali kwa matumizi ya viwandani hutengenezwa Athi River pia.
  • Vifaa na madawa ya ujenzi hutolewa kama gundi la keramiki na mengine

ARM inajenga kituo cha umeme cha makaa chenye nafasi ya megawati 29 huko Kaloleni/Mombasa kwa shabaha ya kupunguza gharama zake za nishati na kuuza umeme wa ziada kwenye soko la kitaifa.

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]