Arakinida

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Arakinida
Buibui ni oda ndani ya arakinida
Buibui ni oda ndani ya arakinida
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Arthropodi (Wanyama wenye mwili wa pingili na miguu ya kuunga wasio na utimgongo kama wadudu, nge, buibui)
Ngeli: Arakinida (buibui, nge, kaa mkia mshale, chawa)
Ngazi za chini

Kuna oda za


Arakinida ni ngeli ya wanyama wasio na utimgongo. Kiasi wanafana na wadudu lakini wana miguu nane badala ya sita. Katika uainishaji wa kisayansi wamepangwa kama oda kati ya arithropoda.

Aina kati yao zinazojulikana zaidi ni buibui pamoja nge na visulisuli. Wadogo kati yao ni kupa na funduku.

Miili huwa na pande mbili ambayo ni kichwa pamoja na kidari mbele na tumbo nyuma. Ila tu kwa funduku pande zote mbili hazionekani vizuri maadamu zimekua kama sehmu moja. Tabia inayoonekana vizuri ni miguu nane. Hata hapa funza za funduku wengi wana miguu sita tu.

Aina nyingi huwa na miiba ya sumu inayoweza kuuma. Kazi yake ni kusaidia uvindaji wa wanyama wengine lakini kwa spishi kadhaa sumu ni hatari hata kwa viumbe vikubwa kama binadamu akidungwa.


Commons-logo.svg
Wikimedia Commons ina media kuhusu:


Kigezo:Mbegu-biologia

Crystal Clear app babelfish.png Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Arakinida kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.