Matumizi mabaya ya dawa : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
Ukurasa ulianzishwa kwa kuandika '{{see also|Tatizo la kiakili linalosababisha matumizi mabaya ya dawa ili kuathiri hisia za mtu}} {{about|Matumizi ya dawa kwa lengo lisilofaa|albamu ya Dice|Mat...'
(Hakuna tofauti)

Pitio la 12:43, 12 Desemba 2018

Kigezo:Infobox medical condition (new) Matumizi mabaya ya dawa, inayojulikana pia kama matumizi ya dawa kwa lengo lisilofaa, ni mfumo wa matumizi ya dawa ambapo mtumiaji hutumia dawa kwa viwango au kwa mbinu ambazo zinaweza kuwadhuru au kudhuru wengine, na ni aina ya tatizo la kiakili linalohusiana na dawa. Maelezo yanayotofautiana sana kuhusu matumizi ya dawa kwa lengo lisilofaa yanatumika katika miktadha ya afya ya umma, matibabu na haki ya jinai. Katika hali nyingine tabia ya kijinai au tabia ya kibinafsi hutokea mtu akiwa chini ya athari ya dawa, na mabadiliko ya tabia za kipekee za mtu binafsi kwa muda mrefu yanaweza pia kutokea.[1] Kwa kuongezea madhara ya kimwili, kijamii na kisaikolojia, matumizi ya dawa nyingine pia yanaweza kusababisha adhabu za kijinai, ijapokuwa hutosautiana sana kwa kutegemea sheria za nchi husika.[2]

Dawa ambazo mara nyingi huhusiana na istilahi hii ni pamoja na pombe, bangi, dawa za kuleta utulivu na usingizi (barbiturates), dawa za kutibu wasiwasi na hofu (benzodiazepini), kokeini, dawa za kuleta utulivu na usingizi (methaqualone), opioid na baadhi ya substituted amphetamines. Chanzo kamili cha matumizi mabaya ya dawa haijulikani vizuri, huku nadharia mbili zinazotawala zikiwa: ama mpangilio wa jenetiki unaosomwa kutoka kwa wengine, au tabia ambapo mazoea yakikua, hujionyesha kama ugonjwa hatari sana wa kudhoofisha.[3]

Mwaka wa 2010, karibu 5% ya watu (milioni 230) walitumia dawa haramu. [4] Kwa hao watu milioni 27 wana hatari ya juu ya matumizi ya dawa vinginevyo inayojulikana kama matumizi ya dawa kwa kurudia yanayosababisha madhara kwa afya yao, shida za kisaikolojia, au shida za kijamii ambazo huwaweka kwa hatari ya majanga hayo.[4][5] Mwaka wa 2015 matatizo ya kiakili yanayosababisha matumizi mabaya ya dawa ili kuathiri hisia za mtu yalisababisha vifo 307,4000, kutoka vifo 165,000 mwaka wa 1990.[6][7] Kwa haya, idadi kubwa ni za matatizo ya utumiaji wa pombe kwa 137,500, matatizo ya utumiaji wa opioid kwa vifo 122, 100, matatizo ya utumiaji wa amphetamine kwa vifo 12,200, na matatizo ya utumiaji wa kokeini kwa 11,000.[6]


See also

References

  1. Ksir, Oakley Ray; Charles (2002). Drugs, society, and human behavior (toleo la 9th). Boston [u.a.]: McGraw-Hill. ISBN 0072319631.{{cite book}}: CS1 maint: multiple names: authors list (link)
  2. (2002). Mosby's Medical, Nursing & Allied Health Dictionary. Sixth Edition. Drug abuse definition, p. 552. Nursing diagnoses, p. 2109. ISBN 0-323-01430-5.
  3. "Addiction is a Chronic Disease". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 24 Juni 2014. Iliwekwa mnamo 2 Julai 2014. {{cite web}}: Unknown parameter |deadurl= ignored (|url-status= suggested) (help)CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. 4.0 4.1 "World Drug Report 2012" (PDF). UNITED NATIONS. Iliwekwa mnamo 27 Septemba 2016.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  5. "EMCDDA | Information on the high-risk drug use (HRDU) (formerly 'problem drug use' (PDU)) key indicator". www.emcdda.europa.eu. Iliwekwa mnamo 2016-09-27.
  6. 6.0 6.1 GBD 2015 Mortality and Causes of Death, Collaborators. (8 Oktoba 2016). "Global, regional, and national life expectancy, all-cause mortality, and cause-specific mortality for 249 causes of death, 1980–2015: a systematic analysis for the Global Burden of Disease Study 2015". Lancet. 388 (10053): 1459–1544. doi:10.1016/S0140-6736(16)31012-1. PMC 5388903. PMID 27733281. {{cite journal}}: |first1= has generic name (help)CS1 maint: date auto-translated (link) CS1 maint: numeric names: authors list (link)
  7. GBD 2013 Mortality and Causes of Death, Collaborators (17 Desemba 2014). "Global, regional, and national age-sex specific all-cause and cause-specific mortality for 240 causes of death, 1990–2013: a systematic analysis for the Global Burden of Disease Study 2013". Lancet. 385: 117–71. doi:10.1016/S0140-6736(14)61682-2. PMC 4340604. PMID 25530442. {{cite journal}}: |first1= has generic name (help)CS1 maint: date auto-translated (link) CS1 maint: numeric names: authors list (link)

External links

Kigezo:Medical resources

Wikimedia Commons ina media kuhusu:

Kigezo:Abuse