Soka kwa ajili ya Urafiki
Soka kwa ajili ya Urafiki ni mpango wa kila mwaka wa watoto wa kimataifa unaotekelezwa na PJSC Gazprom. Lengo la programu ni kukuza maadili ya vijana na kuwa na shauku ya kujenga afya kupitia soka[1]. Katika mfumo wa programu hii, wachezaji wa mpira wa miguu wenye umri wa miaka 12 kutoka nchi mbalimbali[2] hushiriki katika jukwaa la watoto la kimataifa, Kombe la Dunia katika "Soka kwa ajili ya Urafiki", Siku ya Kimataifa ya Soka na Urafiki[3]. Programu inawezeshwa na FIFA, UEFA, UN, Kamati za Olimpiki na Paralympic, serikali na vyama vya soka vya nchi mbalimbali, Wafadhili wa Kimataifa, taasis za umma, vilabu vya soka vinavyoongoza ulimwenguni[4]. Mratibu wa kimataifa wa programu hii ni Shirika la mawasiliano la AGT (Urusi).[5]
Historia
[hariri | hariri chanzo]Soka kwa ajili ya Urafiki 2013
[hariri | hariri chanzo]Jukwaa la kwanza la kimataifa la Soka kwa ajili ya Urafiki la watoto lilifanyika tarehe 25 Mei 2013, huko London. Watoto 670 kutoka nchi 8 walishiriki: kutoka Bulgaria, Uingereza, Hungaria, Ujerumani, Ugiriki, Urusi, Serbia na Slovenia. Urusi iliwakilishwa na timu 11 za mpira wa miguu kutoka majiji 11 ambayo yataandaa mechi za Kombe la Dunia la FIFA mwaka 2018. Timu za watoto za Zenit, Chelsea, Schalke 04, vilabu vya Crvena Zvezda, washindi wa siku ya michezo ya watoto wa Gazprom na washindi wa tamasha ya Fakel pia walishiriki kwenye jukwaa hilo.[6]
Wakati wa jukwaa, watoto walizungumza na wenzao kutoka nchi nyingine na wanasoka maarufu na pia walihudhuria fainali ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya mwaka 2012/2013 katika uwanja wa Wembley.[7]
Matokeo ya jukwaa ilikuwa barua ya wazi ambayo watoto waliunda viwango vinane vya programu: urafiki, usawa, haki, afya, amani, uaminifu, ushindi na mila. Baadaye barua hiyo ilipelekwa kwa wakuu wa UEFA, FIFA na IOC[8]. Mwezi Septemba 2013, wakati wa mkutano na Vladimir Putin na Vitaly Mutko, Sepp Blatter alithibitisha kupokea barua na kusema kuwa alikuwa tayari kuisaidia programu ya Soka kwa Urafiki.[9]
Soka kwa ajili ya Urafiki 2014
[hariri | hariri chanzo]Kipindi cha pili cha programu ya Soka kwa ajili ya Urafiki kilifanyika Lisbon tarehe 23-25 Mei, 2014 na kushirikisha vijana zaidi ya 450 kutoka nchi 16: Belarus, Bulgaria, Uingereza, Hungaria, Ujerumani, Italia, Uholanzi, Poland, Ureno, Urusi , Serbia, Slovenia, Uturuki, Ukraine, Ufaransa na Kroatia. Wachezaji vijana walishiriki katika jukwaa la kimataifa la Soka kwa ajili ya Urafiki, mashindano ya soka la mtaani na walihudhuria fainali ya Ligi ya Mabingwa wa Barani Ulaya mwaka 2013/2014.[10]
Mshindi wa mashindano ya Kimataifa ya Soka la Mtaani mwaka 2014 ilikuwa timu ya Benfica (Ureno). [10]
Matokeo ya msimu wa pili wa programu ulikuwa uchaguzi wa kiongozi wa harakati za Soka kwa Urafiki. Alikuwa Felipe Suarez kutoka Ureno. Mwezi Juni 2014, kama kiongozi wa harakati, aliyatembelea mashindano ya kimataifa ya tisa ya soka la vijana ili kumbukumba Yuri Andreyevich Morozov.[11]
Soka kwa ajili ya Urafiki 2015
[hariri | hariri chanzo]Msimu wa tatu wa programu wa kimataifa wa Soka kwa ajili ya Urafiki ulifanyika Juni 2015 huko Berlin. Washiriki vijana kutoka bara la Asia - timu za soka za watoto kutoka Japan, China na Kazakhstan - walishiriki katika programu hiyo kwa mara ya kwanza. Kwa ujumla, timu za vijana kutoka vilabu vya mpira wa miguu 24 kutoka nchi 24 zilishiriki katika msimu wa tatu.[12]
Wachezaji vijana walizungumza na wenzao kutoka nchi nyingine na nyota wa soka duniani, ikiwa ni pamoja na balozi wa kimataifa wa programu, Franz Beckenbauer na pia kushiriki katika mashindano ya kimataifa ya soka la mtaani miogoni mwa timu za watoto. Mshindi wa mashindano ya Kimataifa ya Soka mwaka 2015 ilikuwa timu ya watoto ya Rapid (Austria).[13]
Matukio ya msimu wa tatu wa Soka kwa Urafiki yaliandikwa na waandishi wa habari wapatao 200 kutoka kwenye machapisho yanayoongoza duniani na waandishi wa habari 24 wa Ulaya na Asia, ambao walikuwa wanachama wa Kituo cha Kimataifa cha Habari cha Watoto.[13]
Mwisho wa 2015 ilikuwa sherehe ya kutoa tuzo ya Kombe la tunu Tisa, ambalo lilinyakuliwa na klabu ya soka ya Barcelona (Hispania). Mshindi alichaguliwa na watoto ambao, mwishoni mwa jukwaa, walishiriki katika tukio la dunia la kupiga kura lililofanyika katika nchi zote 24 zilizoshiriki.[13]
Mwishoni mwa Jukwaa, washiriki wote walifuatilia utamaduni wa kuhudhuria fainali ya Mabinwa Barani Ulaya 2014/2015 katika uwanja wa Olimpiki huko Berlin.[14]
Soka kwa ajili ya Urafiki 2016
[hariri | hariri chanzo]Mwanzo wa Programu ya Kijamii ya Watoto ya Soka kwa ajili ya Urafiki mwaka 2016 ilitolewa kama sehemu ya mkutano wa waandishi wa habari mtandaoni kupitia Hangout, uliofanyika Machi 24 huko Munich uliohudhuriwa na balozi wa kimataifa wa programu ya Franz Beckenbauer.[15]
Katika msimu wa nne wa programu, timu mpya 8 za watoto kutoka Azerbaijan, Algeria, Armenia, Argentina, Brazili, Vietnam, Kyrgyzstan na Syria zilijiunga, kwa hiyo jumla ya nchi zinazoshiriki kufika 32.[16]
Tarehe 5 Aprili, 2016 zilipigwa kura kwa ajili ya kombe la kipekee, Kombe la Tunu Tisa lilianza. Mashabiki kutoka duniani kote walishiriki katika kuchagua mshindi, lakini uamuzi wa mwisho ulifanywa na washiriki wa programu ya Soka kwa Urafiki kwa kupiga kura. Kombe lilinyakuliwa na kilabu cha mpira wa miguu cha Bayern (Munich). Washiriki katika Soka kwa ajili ya Urafiki walibainisha shughuli za kilabu ili kusaidia watoto wenye mahitaji maalum, pamoja na mipango ya kutoa matibabu kwa watoto katika nchi mbalimbali na kuwasaidia wale wanaohitaji.[17]
Jukwaa la nne la kimataifa la watoto wa Soka kwa ajli ya Urafiki na mchezo wa mwisho wa mashindano ya kimataifa ya soka la watoto wa mtaani yalifanyika Mei 27-28, 2016 huko Milan. Mshindi wa mashindano ilikuwa timu ya Maribor kutoka Slovenia. Mwishoni mwa Jukwaa, washiriki walifuata utamaduni wa kuhudhuria fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Matukio ya Jukwa yaliandikwa na waandishi wa habari zaidi ya 200 kutoka vyombo vya habari vinavyoongoza duniani, pamoja na Kituo cha Habari cha Kimataifa cha Watoto, kilichojumuisha waandishi wa habari vijana kutoka nchi zinazoshiriki.[18]
Wachezaji vijana kutoka klabu ya Syria ya Al-Wahda walishiriki katika msimu wa nne wa Soka kwa ajili ya Urafiki, ambayo ilikuwa haijawahi kutokea. Kuingizwa kwa timu ya Syria kati ya washiriki wa programu na ziara ya watoto wa Syria katika jukwaa huko Milan ilikuwa hatua muhimu kukabiliana na kutengwa kwa binadamu wa nchini hiyo. Bodi ya uhariri wa michezo ya Kiarabu ya kituo cha kimataifa cha televisheni Russia Today, kwa msaada wa Shirikisho la Soka la Siria, lirekodi filamu ya makala "Siku tatu bila vita" kuhusu watoto walioshiriki katika mradi huo. Tarehe 14 Septemba 2016, zaidi ya watu 7,000 walitembelea tamasha ya filamu huko Damascus.[19]
Soka kwa ajili ya Urafiki 2017
[hariri | hariri chanzo]Viwango vya mradi wa kimataifa wa kijamii wa watoto wa Soka kwa ajili ya Urafiki mwaka 2017 ulifanyika St. Petersburg (Urusi) na matukio ya mwisho yalifanyika hapa taree 26 Juni hadi 3 Julai.[20]
Mwaka 2017, idadi ya nchi zinazoshiriki iliongezeka kutoka 32 hadi 64. Kwa mara ya kwanza, programu ya Soka kwa ajili ya Urafiki ilihudhuriwa na watoto kutoka Meksiko na Marekani. Hivyo, mradi huo uliunganisha wachezaji vijana wa mabara manne - Afrika, Ulaya-Asia, Amerika ya Kaskazini na Amerika ya Kusini.[21]
Katika msimu wa tano programu hiyo ilitekelezwa kwa kuzingatia dhana mpya: mchezaji mmoja mdogo kutoka kila nchi alichaguliwa kuiwakilisha nchi hiyo. Vijana waliungana katika Timu nane za Urafiki za Kimataifa, zilizoundwa na wavulana na wasichana wenye miaka 12, ikiwa ni pamoja na wale wenye ulemavu.[22]
Wakati wa droo ya wazi, muundo wa timu wa nchi na nafasi za mchezo kwa wawakilishi wa nchi zinazohusika uliamua. Droo ilifanyika kwenye mkutano wa mtandaoni. Katika uongozi wa timu nane za Timu za Urafiki walikuwa makocha vijana: Rene Lampert (Slovenia), Stefan Maksimovich (Serbia), Brandon Shabani (Uingereza), Charlie Sui (China), Anatoly Chentuloyev (Urusi), Bogdan Krolevetsky (Urusi), Anton Ivanov (Urusi), Emma Henschen (Uholanzi). Liliya Matsumoto (Japani), mwakilishi wa kituo cha kimataifa cha wanahabari cha Soka kwa Urafiki, pia alishiriki katika droo.[23]
Mshindi wa Kombe la Dunia wa Soka kwa ajili ya Urafiki 2017 ilikuwa timu ya "Orange", ambayo ilikuwa na kocha kijana na wachezaji wa soka vijana kutoka nchi tisa: Rene Lampert (Slovenia), Hong Jun Marvin Tue (Singapore), Paul Puig I Montana (Hispania) ), Gabriel Mendoza (Bolivia), Ravan Kazimov (Azerbaijan), Khrisimir Stanimirov Stanchev (Bulgaria), Ivan Agustin Casco (Argentina), Roman Horak (Jamhuri ya Cheki), Hamzah Yusuf Nuri Alhavvat (Libya).
Jukwaa la kimataifa la watoto la Soka kwa ajili ya Urafiki liliudhuriwa na Viktor Zubkov (mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa PJSC Gazprom)[24], Fatma Samura (katibu mkuu wa FIFA), Philippe Le Flock (mkurugenzi mkuu wa FIFA), Giulio Baptista (Mchezaji wa soka wa Brazil), Ivan Zamorano (mshambuliaji wa Chile), Alexander Kerzhakov (mchezaji wa Urusi) na wageni wengine, ambao walihimiza kukuza maadili ya binadamu muhimu miongoni mwa vijana[25].
Mwaka 2017, mradi huo uliwashirikisha watu zaidi ya 600,000, na zaidi ya watoto 1,000 na watu wazima kutoka nchi 64 walihudhuria matukio ya mwisho huko St. Petersburg.[26]
Soka kwa ajili ya Urafiki 2018
[hariri | hariri chanzo]Mwaka 2018, iliamuliwa kwamba Msimu wa Sita wa Programu ya Mpira wa Miguu kwa Ajili ya Urafiki ulifanyika kuanzia Februari 15 hadi Juni 15. Tukio la kutamatisha shughuli hizo lilifanyika Moscow muda mfupi kabla ya Kombe la Dunia 2018. Washiriki wa Programu hii ni pamoja na wanasoka na wanahabari vijana wanaowakilisha nchi na kanda 211 duniani. Kuanza rasmi kwa Programu ya mwaka 2018 ilifanyika kwa Droo ya Wazi iliyokuwa mubashara ya Mpira wa Miguu kwa Ajili ya Urafiki, ambapo timu 32 za kimataifa za mpira wa miguu – Timu za Urafiki[27] – ziliundwa.
Kwa kuhusisha na harakati za mazingira, Timu za Mpira wa Miguu za Kimataifa za Urafiki za 2018 zilipewa majina ya aina ya wanyama adimu na walio hatarini.
Pia, ndani ya mfumo wa harakati za mazingira, Kampeni ya Kimataifa ya Happy Buzz Day kuhamasisha jumuiya ya kimataifa kusaidia asasi zinazojishughulisha na kuokoa viumbe vilivyo hatarini ilizinduliwa Mei 30, 2018. Hifadhi za taifa na mbuga za akiba za Urusi, Marekani, Nepal na Uingereza[28] zilijiunga na Kampeni.
Aidha, wakati wa shughuli za mwisho za Programu ya Mpira wa Miguu kwa Ajili ya Urafiki mjini Moscow, washiriki walisafiri kwa mabasi rafiki kwa mazingira yanayotumia gesi ya asili[29].
Timu 32 za Kimataifa za Urafiki zilishiriki katika Mashindano ya Kimataifa ya Mpira wa Miguu kwa Ajili ya Urafiki ya 2018. Kwa mara ya kwanza katika historia ya Programu hii, mechi ya mwisho ilitangazwa na mtangazaji kijana kutoka Syria, Yazan Taha [87] na kuchezeshwa na Mwamuzi Kijana wa Urusi, Bogdan Batalin[30].
Mshindi wa Mashindano ya Kimataifa ya Mpira wa Miguu kwa Ajili ya Urafiki ya 2018 ilikuwa timu ya "Sokwe" inayojumuisha Wachezaji Vijana kutoka Dominika, St. Kitts na Nevis, Malawi, Colombia, Benin na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Vladislav Poliakov[31], Mshiriki Kijana wa Saransk, Urusi, alikuwa kocha wa timu.
Tukio la mwisho la Msimu wa Sita wa Programu hii likawa Jukwaa la Mpira wa Miguu la Kimataifa la Watoto kwa ajili ya Urafiki la 2019, lililofanyika Juni 13 katika Kituo cha Mambo ya Bahari na Biolojia ya bahari "Moskvarium". Lilihudhuliwa na Viktor Zubkov (Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Gazprom), Olga Golodets (Naibu Mwenyekiti wa Serikali ya Shirikisho la Urusi), Iker Casillas (Mchezaji wa Uhispania, ahodha wa zamani wa timu ya taifa), Aleksandr Kerzhakov (mchezaji wa Kirusi, mwalimu wa timu ya vijana ya Urusi), vile vile wawakilishi wa balozi 54 duniani kote na wageni wengine[32].
Wakati Jukwaa, Wachezaji bora Vijana wa Msimu wa Sita walizawadiwa: Deo Kalenga Mwenze kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (mshambuliaji bora), Yamiru Ouru kutoka Benin (kiugo bora), Ivan Volynkin kutoka Wales (kipa bora) na Gustavo Cintra Rocha kutoka Brazil (MVP)[33].
Sakali Ascension kutoka Aruba alikuwa Mwandishi wa Habari Kijana wa 2018 wa Programu ya Mpira wa Miguu kwa Ajili ya Urafiki, alishughulikia blogu ambayo ilikuwa inahamasisha vijana wa Oceania kuwa na ufahamu zaidi wa mazingira[33].
Pia jukwaa liliandaa uwasilishaji wa kitabu na muda wa kuweka sahihi kutakofanywa na mshiriki wa Msimu uliopita, Ananya Kamboj[34] kutoka India. Ananya aliandika kitabu "My journey from Mohali to St. Petersburg" baada ya Msimu wa Tano wa Mpira wa Miguu kwa ajili ya Urafiki wa 2017, akielezea uzoefuwake kama Mwanahabari Kijana. Hapo aliandika kuhusu Kanuni Tisa za Programu, ambazo zinasaidia kuubadilisha ulimwengu kwa nia njema.
Juni 14, baada ya Jukwaa la Kimataifa la Mpira wa Miguu wa Watoto kwa Ajili ya Urafiki la 2018, Wachezaji na Wanahabari Vijana walishiriki katika sherehe za ufunguzi wa Kombe la Dunia la FIFA la 2018 nchini Urusi. Katika uwanja wa "Luzhniki", watoto kwa taadhima walipeperusha bendera za nchi na kanda zote 211 zilizoshiriki katika Programu za mwaka huo[35]. Baada ya hapo, Vijana Washiriki wa Mpira wa Miguu kwa Ajili ya Urafiki walitazama mchezo wa ufunguzi kati ya timu ya Urusi na Saudi Arabia.
Rais wa Shirikisho la Urusi Vladimir Putin alimualika Balozi Kijana wa Urusi wa Mpira wa Miguu kwa Ajili ya Urafiki Albert Zinnatov kwenye jukwaa maalum ili kuangalia mechi ya ufunguzi pamoja. Pale kijana alipata fursa ya kuzugumza na Mshindi wa Kombe la Dunia kutoka Brazil Roberto Carlos na mchezaji wa soka wa Kihispaniola Iker Casillas[36].
Zaidi ya watoto na vijana 1500 kutoka nchi na kanda 211 walikuwa washiriki wa tukio la mwisho lililofanyika Moscow. Kwa ujumla, zaidi ya matukio 180 yaliyoshirikisha vijana zaidi ya 240,000[37] yaliratibiwa katika Msimu wa Sita katika kanda mbalimbali duniani.
Mwaka 2018, wawakilishi wa Mamlaka waliunga mkono mradi huo. Olga Golodets alisoma hotuba ya ukaribisho kutoka kwa Rais wa Urusi Vladimir Putin kwa washiriki na wageni wa Jukwaa la Kimataifa la Watoto[38].
Mwenyekiti wa Serikali ya Shirikisho la Urusi Dmitry Medvedev alituma ujumbe wa ukaribisho kwa njia ya telegram kwa washiriki na wageni wa Jukwaa la sita la Kimataifa la Watoto la Mpira wa Miguu kwa Ajili ya Urafiki[39].
Wakati wa mkutano Mei 23, Mwakilishi Rasmi wa MIA ya Urusi Maria Zakharova alieleza kwamba jumuiya ya kimataifa inaitambua Programu ya Mpira wa Miguu kwa Ajili ya Urafiki ya siku hizi kama sehemu muhimu ya masuala ya kibinadamu ya sera ya kimataifa ya kijamii ya Urusi[39].
FIFA iliungamkono kiasili Programu ya Mpira wa Miguu kwa Ajili ya Urafiki. Shirika lilibaini kwamba idadi kamili ya washiriki na wageni wa matukio ya mwisho yaliyofanyika Moscow ilifika watu 5000[40].
Soka kwa ajili ya Urafiki 2019
[hariri | hariri chanzo]Ufunguzi wa msimu was saba wa Programu ya Kijamii ya Watoto ya Kimataifa «Soka kwa Urafiki» umefanyika Machi 18 mwaka 2019, matukio ya fainali ya programu hiyo zilifanyika huko Madrid kuanzia Mei 28 hadi Juni 2.[41]
Siku ya Kimataifa ya Soka na Urafiki Aprili 25 iliadhimishwa katika nchi zaidi ya 50 za Ulaya, Asia, Afrika, Amerika ya Kaskazini na Kusini. Ushirika wa Soka wa Urusi (RFS) pia ulishiriki katika sherehe hiyo.[42]
Tarehe Mei 30 huko Madrid jukwaa la kimataifa la Programu ya Kijamii ya Watoto linalotekelezwa na PJSC Gazprom «Soka kwa ajili ya Urafiki» mwaka 2019. Jukwaa hilo liliunganisha wataalamu kutoka ulimwenguni kote yaani makocha ya soka, madaktari wa timu za kitoto, nyota wengi wa kimataifa, wanahabari wa vyombo vya habari bora vya kimataifa, wajumbe wa shule za mpira na mashirikisho ya mpira za kimataifa.[43]
Tarehe Mei 31 huko Madrid matayarisho ya kimataifa sana yamefanyika. Kisha «Soko kwa ajili ya Urafiki» imepata cheti rasmi cha GUINNESS WORLD RECORDS®.[44]
Wakati wa msimu wa saba, waandishi wachanga wa habari 32 kutoka Ulaya, Afrika, Asia, Amerika ya Kaskazini na Kusini waliunda muundo wa kituo cha waandishi wa habari cha watoto wa kimataifa cha «Soko kwa ajili ya Urafiki», ambao uliangazia matukio ya fainali ya programu hiyo na kushiriki katika utayarishaji wa makala pamoja na vyombo vya kimataifa na kitaifa.[45]
Washiriki wa msimu wa saba walikabidhi Kombe la Thamani Tisa (tuzo ya programu ya kijamii ya watoto ya kimataifa «Soko kwa ajili ya Urafiki») kwa Klabu ya Soka ya Liverpool kama timu inayohusika zaidi kijamii.[46]
Tarehe Juni 1, tukio kuu la msimu wa saba, mechi ya fainali ya Kombe la Dunia la Soka kwa ajili ya Urafiki, lilifanyika kwenye uwanja wa UEFA Pitch huko Madrid. Kulingana na matokeo yake, timu ya Nyoka ya Antiguan ilicheza na Tasmanian Devil na magoli ya 1:1 kwa wakati wa kawaida, na kisha kushinda kwa mikwaju ya penati na kupata tuzo kuu.[47]
Soka kwa ajili ya Urafiki 2020
[hariri | hariri chanzo]Mwaka 2020 matukio ya fainali ya msimu wa nane wa «Soko kwa ajili ya Urafiki» yamefanyika online kwenye jukwaa la kidigitali kuanzia Novemba 27 hadi Desemba 9 mwaka 2020. Washiriki zaidi ya 10 000 kutoka nchi 100 walijiunga na matukio makuu.[48]
Kwa msimu wa nane wa programu hiyo, simulator ya soka mtandaoni «Soka kwa ajili ya Urafiki» kwa wachezaji wengi ilitengenezwa, kwa msingi ambao Mashindano ya Soka ya Kimataifa ya 2020 yalifanyika. Mchezo unapatikana kwa kupakuliwa ulimwenguni kote tangu Desemba 10, 2020 - Siku ya Soka Duniani. Watumiaji wana nafasi ya kushiriki kwenye mechi kulingana na sheria za «Soka kwa ajili ya Urafiki», kuungana katika timu za kimataifa. Mchezo wa wachezaji wengi unategemea maadili ya msingi ya programu, kama vile urafiki, amani na usawa.[49]
Novemba 27 kinyang'anyiro cha hadhira cha Mashindano ya ulimwengu mkondoni «Soka kwa ajili ya Urafiki» 2020 kimefanyika[50]
Kuanzia Novemba 28 hadi Desemba 6 kambi la kimataifa la urafiki mkondoni na mipango ya elimu ya kibinadamu na michezo kwa watoto limefanyika.[51]
Kuanzia Novemba 30 hadi Desemba 4 vikao vya jukwaa la kimataifa mkondoni «Soka kwa ajili ya Urafiki» vilifanyika, ambapo miradi katika ukuzaji wa michezo ya watoto iliwasilishwa. Juri la wataalam lilithamini uwasilishaji wa miradi kwa tuzo ya kimataifa «Soka kwa ajili ya Urafiki»[52]
Desemba 7-8 Ubingwa wa mtandaoni wa kimataifa wa «Soka kwa ajili ya Urafiki» umefanyika. Mwaka huu, ubingwa ulifanyika kwenye jukwaa la kidigitali, kwa hivyo simulator ya mpira «Soka kwa ajili ya Urafiki» kwa wachezaji wengi ilitengenezwa.[53]
Desemba 9 fainali kubwa ya «Soka kwa ajili ya Urafiki» imefanyika.[54]
Mfululizo wa webinars kwa watoto kutoka nchi nyingi kutokana na miaka 75 ya Umoja wa Mataifa ulifanyika wakati wa msimu huu wa nane.[55]
Wakati wa msimu huu wa nane wa programu hii pamoja na freestylers wa mpira kutoka duniani kote show ya kila wiki «Uwanja upo ndipo nipo» imezinduliwa. Katika kila kipindi freestylers waliwafundisha wachanga kufanya mazoezi, na mwishoni mwa kila vipindi kila mashindano yalitangazwa kwa utendaji bora wa zoezi. Show ilimalizika na darasa la ulimwengu la mkondoni, ambalo programu ya «Soka kwa ajili ya Urafiki» ukawa mshindi wa Rekodi ya Dunia ya Guinness kwa mara ya pili kwa idadi ya washiriki waliohusika (Desemba 6 mwaka 2020).[56]
Wahariri wa Habari Njema – show ya kila wiki lililozinduliwa na waandishi wa habari wachanga wa «Soka kwa ajili ya Urafiki», ambapo watoto walipashana habari njema kutoka ulimwenguni kote na watazamaji[57]
Michuano ya Dunia ya Soka kwa Urafiki
[hariri | hariri chanzo]Mashindano ya soka ya kimataifa ya watoto yanafanyika ndani ya mfumo wa programu ya Soka kwa Urafiki. Timu zinazoshiliki katika michuano - Timu za Urafiki - huundwa wakati wa Droo ya Wazi. Timu hizo zimeandaliwa kwa kufuata kanuni za Soka kwa Urafiki: wanariadha wa mataifa tofauti, jinsia na utimamu wa mwili hucheza katika timu moja.[58]
Jukwaa la Kimataifa la Watoto la Soka kwa Urafiki
[hariri | hariri chanzo]Katika Jukwaa la Kimataifa la Watoto la Soka kwa Urafiki, washiriki vijana mradi hujadili na watu wazima juu ya kukuza na kuvistawisha viwango vya programu duniani kote. Wakati wa Jukwaa, watoto hukutana na kuzungumza na wenzao kutoka nchi nyingine, wanasoka maarufu, waandishi wa habari na watu mashuhuri, na pia kuwa mabalozi vijana ambao baadaye huendeleza maadili mame kwa wenzao.[59]
Kituo cha Waandishi wa Kimataifa cha Watoto
[hariri | hariri chanzo]Kipengele maalum cha programu ya Soka kwa Urafiki ni Kituo chake cha Kimataifa cha Waandishi wa Habari cha Watoto. Kwa mara ya kwanza kiliandaliwa chini ya programu ya Soka kwa Urafiki mwaka 2014[60]. Waandishi wa habari vijana katika kituo cha waandishi wa habari huandika matukio ya programu kwaa nchi zao[61]: huandaa habari kwa vyombo vya habari vya kitaifa na kimataifa, kushiriki katika kuundwa vifaa kwa ajili ya kituo cha Televisheni cha Soka kwa Urafiki, gaziti la watoto la Urafiki kwa Urafiki na kituo rasmi cha redio cha programu[62]. Kituo cha Kimataifa cha Waandishi wa Habari cha Watoto kinaunganisha washindi wa mashindano ya kitaifa ya Waandishi wa Habari Vijana[63], wanablogu vijana, wapiga picha na waandishi. Waandishi wa habari vijana wa kituo cha waandishi wa habari hutoa maoni yao kutoka ndani ya programu, kutekeleza muundo "watoto kuhusu watoto".[64]
Siku ya Kimataifa ya Soka na Urafiki
[hariri | hariri chanzo]Chini ya programu ya Soka kwa Urafiki, Siku ya Kimataifa ya Soka kwa Urafiki husherekewa tarehe 25 Aprili[65]. Katika mapumziko haya iliadhimishwa kwa mara ya kwanza mwaka 2014 katika nchi 16[66]. Katika siku hii, mechi za kirafiki, mobs flash, mbio ndefu, madarasa ya sanaa, maonyesho ya televisheni, vikao vya mafunzo ya wazi, nk. hufanyika. Watu zaidi ya 50,000 hushiriki katika maadhimisho hayo.[67]
Mwaka 2015, Siku ya Soka na Urafiki iliadhimishwa katika nchi 24[68]. Wakati wa tamasha hilo, kulikuwa na mechi za soka za kirafiki na matukio mengine. Ujerumani, wanasoka wa Schalke 04 walitoa mafunzo ya wazi[69], Serbia iliandaa maonyesho ya televisheni, Ukraine - mechi kati ya timu watoto ya Volyn FC na watoto waliosajiliwa katika kituo cha mji wa Lutsk cha huduma za kijamii kwa familia, watoto na vijana.[70]
Urusi, Siku ya Soka na Urafiki iliadhimishwa Aprili 25 katika katika majiji 11. Mechi za soka za kirafiki zilifanyika Vladivostok, Novosibirsk, Yekaterinburg, Krasnoyarsk, Barnaul, St. Petersburg na Saransk, kukumbuka viwango muhimu ya programu. Krasnoyarsk, Sochi na Rostov-on-Don, Urafiki wa Kupokezana ulifanyika kwa ushiriki wa wakimbiza mwenge kutoka kwenye Kupokezana Mwenge wa Olimpiki 2014. Moscow, kwa msaada wa Shirikisho la Michezo la Blind, Mashindano ya Fursa Sawa yaliandaliwa. Tarehe 5 Mei, Siku ya Soka na Urafiki iliadhimishwa huko Nizhny Novgorod na Kazan.[10]
Mwaka 2016, Siku ya Soka na Urafiki iliadhimishwa katika nchi 32. Urusi, iliadhimishwa katika miji tisa: Moscow, St. Petersburg, Novosibirsk, Barnaul, Birobidzhan, Irkutsk, Krasnodar, Nizhny Novgorod na Rostov-on-Don. Nizhny Novgorod aliandaa mechi ya kirafiki kwa wanasoka vijana kutoka Volga FC, na wachezaji watu wazima kutoka klabu hiyo walifanya mazoezi na mafunzo kwa watoto. Katika mechi ya kirafiki huko Novosibirsk, watoto wenye ulemavu walishiriki katika - timu ya mkoa wa Novosibirsk Yermak-Sibir.[17]
Mwaka 2017, Siku ya Soka na Urafiki iliadhimishwa katika nchi 64. Wachezaji mashuhuri, ikiwa ni pamoja na mlinzi wa Serbian Branislav Ivanovich na mshambuliaji wa Kiholanzi Dirk Kuyt, walishiriki katika matukio duniani kote. Nchini Ugiriki, tukio lilihudhuriwa na Theodoras Zagorakis, mshindi wa michuano ya soka ya Ulaya 2004 na timu yake ya taifa. Nchini Urusi, Zenit FC ilihudhuria kipengele cha mafunzo maalum ya Zakhar Badyuk, Balozi mdogo wa programu ya Soka kwa Urafiki mwaka 2017. Katika mafunzo, kipa wa Zenit FC, Yury Lodygin alitoa alama za juu kuelezea uwezo wa Zakhar na kumwelezea siri za ukipa.[23]
Kanuni tisa za Mpira wa Miguu kwa Ajili ya Urafiki
[hariri | hariri chanzo]Wakati wa Jukwaa la Kwanza la Kimataifa la Watoto lililofanyika Mei 25, 2013, Mabalozi Vijana kutoka Uingereza, Ujerumani, Serbia, Hungary, Serbia, Bulgaria, Ugiriki na Urusi waliheshimu kanuni nane za kwanza za Programu - urafiki, usawa, haki, afya, amani, ibada, ushindi, na mila – na waliziwasilisha katika Barua ya Wazi. Barua ilitumwa kwa Wakuu wa Mashirika ya Michezo ya Kimataifa: Shirikisho la Mpira Wa Miguu Duniani (FIFA), Umoja wa Vyama vya Soka Ulaya (UEFA) na Kamati ya Olimpiki ya Kimataifa. Septemba 2013, Joseph Blatter wakati akifanya mkutano na Vladimir Putin na Vitalii Mutko alithibitisha kupokea Barua hiyo na kukubali kwamba yuko teyari kuaidia Mpira wa Miguu kwa Ajili ya Urafiki[11].
Mwaka 2015, washiriki kutoka China, Japan na Kazakhstan walijiunga na Programu ya Mpira wa Miguu kwa ajili ya Urafiki na kisha walipendekeza kuongezwa kanuni ya tisa – sifa njema[71].
Kombe la Viwango Tisa
[hariri | hariri chanzo]Kombe la Viwango Tisa ni tuzo ya Programu ya Kimataifa ya Watoto ya ya Kijamii ya Soka kwa Urafiki. Kila mwaka Kombe linatuzwa kwa kujitolea zaidi kwa maadili ya mradi: urafiki, usawa, haki, afya, amani, uaminifu, ushindi, mila na heshima. Mashabiki kutoka duniani kote hushiriki katika kuchagua mshindi, lakini uamuzi wa mwisho hufanywa na washiriki wa programu ya Soka kwa ajili ya Urafiki kwa kupiga kura. Vilabu vya soka ambavyo ni wamiliki wa Kombe la Viwango Tisa: Barcelona (2015), Bayern Munich (2016), Al Wahda (Tuzo maalum), Real Madrid (2017).[72]
Bangili ya Urafiki
[hariri | hariri chanzo]Shughuli zote za mpango wa Soka kwa ajili ya Urafiki huanza kwa kubadilishana bangili za urafiki, ikiwa ni ishara ya usawa na maisha ya afya. Bangili ina mistari miwili ya rangi ya bluu na kijani na inaweza kuvaliwa na mtu yeyote ambaye anashirikisha wengine viwango vya mpango.
Kwa mujibu wa Franz Beckenbauer
"Ishara ya harakati ni bangili ya rangi mbili, ni rahisi na inayoeleweka kama viwango vya asili vya programu ya Soka kwa Urafiki.
Washiriki vijana katika programu wamefunga Bangili za Urafiki kwenye miono ya wachezaji maarufu na watu mashuhuli[73], ikiwa ni pamoja na: Dick Advocaat[74], Anatoly Timoshchuk[75] na Luis Netu, Franz Beckenbauer[76], Luis Fernandev, Didier Drogba , Max Meyer, Fatma Samura, Leon Gorecka, Domenico Krishito, Michel Salgado, Alexander Kerzhakov, Dimas Pirros, Miodrag Bozovic, Adelina Sotnikova, Yuri Kamenets.
Shughuli za washiriki kati ya misimu
[hariri | hariri chanzo]Vijana wa soka kutoka kwenye programu ya Soka kwa Urafiki hushiriki katika matukio mbalimbali nje ya msimu rasmi. Mwezi Mei 2013, wachezaji kutoka klabu ya mpira wa miguu ya Maribor (Slovenia) walicheza mechi ya kirafiki na watoto wa Cambodian[77]. Tarehe 14, Septemba, 2014 katika mji wa Sochi, washiriki wa Urusi katika programu walizungumza na Vladimir Putin wakati wa mkutano wa Rais wa Shirikisho la Urusi na Rais wa FIFA Sepp Blatter[78]. Juni 2014, Rais wa Ufaransa, Francois Hollande aliialika timu ya Taverni, ambaye ni mwanachama wa programu ya Soka kwa Urafiki, kwenye Elysee Palace kutazama mechi ya Kombe la Dunia la FIFA ya 2014 kati ya Ufaransa na Nigeria[79]. Mwezi Aprili 2016, Yuri Vashchuk, balozi wa programu ya Soka kwa Urafiki wa mwaka 2015, alikutana na mtu mwenye nguvu zaidi wa Belarus, Kirill Shimko, na mwanaoka kijan kutoka BATE FC kubadilishana uzoefu wao wa kushiriki katika mradi huo. Yuri Vashchuk alimpa Kirill Shimko Bangili ya Urafiki wa mfano, na hivyo kumkabidhi kitufu cha kutangaza kauli mbiu za mradi: urafiki, haki, maisha ya afya.
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ https://www.sportindustry.biz/news/football-friendship-project-returns
- ↑ inserbia.info/today/2014/04/gazproms-football-for-friendship-2014
- ↑ www.newswire.ca/en/story/1505319/europe-and-asia-to-meet-within-football-for-friendship-international-children-s-social-project-of-gazprom
- ↑ ""Футбол для дружбы" 2018: объявлены имена участников программы от России!". www.sport-express.ru. 2018-04-25. Iliwekwa mnamo 2019-04-16.
- ↑ www.prnewswire.com/news-releases/young-football-players-from-24-countries-of-europe-and-asia-meet-at-third-international-childrens-football-for-friendship-forum-506472841.html
- ↑ https://archive.today/20150515191023/http:/fcbusiness.co.uk/news/article/newsitem=2379/title=franz+beckenbauer+kicks+off+gazprom%92s+%91football+for+friendship%92+campaign
- ↑ www.ntv.ru/sport/627113
- ↑ https://www.fifa.com/about-fifa/marketing/sponsorship/partners/gazprom.html
- ↑ https://web.archive.org/web/20150522173321/http:/www.epochtimes.de/service/vladimir-putin-und-fifa-praesident-joseph-s-blatte-bei-football-for-friendship-222
- ↑ 10.0 10.1 10.2 www.euronews.com/2014/05/27/football-for-friendship-teaching-values-through-football
- ↑ 11.0 11.1 www.lazionews.eu/settore-giovanile/oltre-450-ragazzi-riuniti-da-gazprom-in-occasione-del-secondo-forum-internazionale-football-for-friendship/
- ↑ www.noodls.com/viewNoodl/28582380/oao-gazprom/young-football-players-from-24-countries-of-europe-and-asia-
- ↑ 13.0 13.1 13.2 www.noodls.com/viewNoodl/28582380/oao-gazprom/young-football-players-from-24-countries-of-europe-and-asia-
- ↑ www.prnewswire.com/news-releases/young-football-players-from-24-countries-of-europe-and-asia-meet-at-third-international-childrens-football-for-friendship-forum-506472841.html
- ↑ www.mirror.co.uk/sport/football/news/franz-beckenbauer-reveals-hes-barcelona-7695610
- ↑ www.sgb-sports.com/index.php/fourth-gazprom-football-for-friendship-project-launches/
- ↑ 17.0 17.1 rbth.com/sport/2016/06/01/gazprom-brings-soccer-crazy-kids-to-milan-for-uefa-champions-league-final_599353
- ↑ www.beyondsport.org/articles/fourth-international-football-for-friendship-forum-brings-together-young-footballers-from-three-continents/
- ↑ www.euronews.com/2016/05/31/football-for-friendship-syrian-youth-team-make-tournament-debut-in-milan
- ↑ www.windsorstar.com/business/cnw/release.html?rkey=20170316C8720&filter=5613
- ↑ finance.dailyherald.com/dailyherald/news/read/33918303/Fifth_Season_of_Gazprom's_Football_for_Friendship_International_Children's_Project_Launched
- ↑ https://www.merrilledge.com/research/story?stryKey=600-201703161740PR_NEWS_USPRX____enUK201703165338-1
- ↑ 23.0 23.1 www.newswit.com/.gen/2017-03-17/bafb838790ea60129b53d1add5e4ee99/
- ↑ https://www.24sata.hr/sport/nogomet-za-prijateljstvo-novi-ciljevi-uz-djecu-iz-64-drzave-531487
- ↑ www.euronews.com/2017/07/06/football-brings-kids-together
- ↑ stomp.straitstimes.com/singapore-seen/12-year-old-sporean-messi-wins-global-football-contest-in-russia
- ↑ RBTH (2015-05-15). "Children from 24 countries celebrate Day of Football and Friendship". www.rbth.com (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2019-04-28.
- ↑ "Газпром Футбол F4F News-Detail". www.gazprom-football.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-04-11. Iliwekwa mnamo 2019-04-28.
- ↑ "Газпром Футбол F4F News-Detail". www.gazprom-football.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-04-11. Iliwekwa mnamo 2019-04-28.
- ↑ "Их подружил футбол". Советский спорт (kwa Kirusi). Iliwekwa mnamo 2019-04-28.
- ↑ "Юный тренер из России стал чемпионом мира по "Футболу для дружбы"". www.sport-express.ru. 2018-06-13. Iliwekwa mnamo 2019-04-28.
- ↑ "Море счастья, дружбы и футбола!". www.sport-express.ru. 2018-06-29. Iliwekwa mnamo 2019-04-28.
- ↑ 33.0 33.1 "Шикарный футбол, крепкая дружба!". Советский спорт (kwa Kirusi). Iliwekwa mnamo 2019-04-28.
- ↑ "Море счастья, дружбы и футбола!". www.sport-express.ru. 2018-06-29. Iliwekwa mnamo 2019-04-28.
- ↑ "Юные послы "Футбола для дружбы" приняли участие в церемонии открытия ЧМ-2018". Спорт РИА Новости (kwa Kirusi). 20180615T2036+0300Z. Iliwekwa mnamo 2019-04-28.
{{cite web}}
: Check date values in:|date=
(help) - ↑ "Юный посол "Футбола для дружбы" встретился с президентом России на ЧМ в Москве". www.sport-express.ru. 2018-06-21. Iliwekwa mnamo 2019-04-28.
- ↑ "Участники "Футбола для дружбы" из 211 стран и регионов прибыли в Москву". www.sport-express.ru. 2018-06-09. Iliwekwa mnamo 2019-04-28.
- ↑ "Участникам и гостям Международного детского форума «Футбол для дружбы»". government.ru (kwa Kirusi). Iliwekwa mnamo 2019-04-28.
- ↑ 39.0 39.1 "Брифинг официального представителя МИД России М.В.Захаровой, Москва, 23 мая 2018 года". www.mid.ru (kwa Kirusi). Iliwekwa mnamo 2019-04-28.
- ↑ FIFA.com. "2018 FIFA World Cup Russia™ - News - 211 countries and regions take part in the Sixth International Football for Friendship Children's Forum - FIFA.com". www.fifa.com (kwa Kiingereza (Uingereza)). Iliwekwa mnamo 2019-04-28.
- ↑ "The Daily Times Leader". business.dailytimesleader.com. Iliwekwa mnamo 2020-12-24.
- ↑ Gazprom Football for Friendship. "International Day of Football and Friendship Celebrated in Schools Around the World". www.prnewswire.com (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2020-12-24.
- ↑ "Int'l Football for Friendship Forum 2019 in Madrid Unites Kids' Soccer Experts From Around the Globe". sputniknews.com (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2020-12-24.
- ↑ "Most nationalities in a football (soccer) training session". Guinness World Records (kwa Kiingereza (Uingereza)). Iliwekwa mnamo 2020-12-24.
- ↑ "Football for Friendship Young Participants became correspondents of international media". TASS. Iliwekwa mnamo 2020-12-24.
- ↑ "End of Seventh Season of Football for Friendship in Madrid". sputniknews.com (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2020-12-24.
- ↑ "Football for Friendship: Sportsmanship has no borders". euronews (kwa Kiingereza). 2019-06-06. Iliwekwa mnamo 2020-12-24.
- ↑ "Gazprom Football For Friendship International Children's Programme | F4F". footballforfriendship.com (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2020-12-24.
- ↑ "New 'Football for Friendship' Simulator to be Released on World Football Day". sputniknews.com (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2020-12-24.
- ↑ "Gazprom Football: Newsdetail". Gazprom Football (kwa Kijerumani). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-12-19. Iliwekwa mnamo 2020-12-24.
- ↑ "Friendship Camp | F4F". footballforfriendship.com (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2020-12-24.
- ↑ "Shortlist | F4F". footballforfriendship.com (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2020-12-24.
- ↑ "World Championship | F4F". footballforfriendship.com (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2020-12-24.
- ↑ "Live Broadcast: Grand Final | F4F". footballforfriendship.com (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2020-12-24.
- ↑ "F4F Ambassadors and FC Schalke 04 discussed the role of football in our future celebrating #UN75 - YouTube". www.youtube.com. Iliwekwa mnamo 2020-12-24.
- ↑ "STADIUM IS WHERE I AM | Easy Learning V-Move With Freestyle Blogger - YouTube". www.youtube.com. Iliwekwa mnamo 2020-12-24.
- ↑ "Good News Show From Young Journalists To Cheer You Up - YouTube". www.youtube.com. Iliwekwa mnamo 2020-12-24.
- ↑ rbth.com/sport/2014/05/30/big_soccer_for_little_europeans_37075.html
- ↑ www.fifa.com/confederationscup/news/y=2017/m=8/news=confed-cup-hosts-friendship-forum-2902692.html
- ↑ www.crawleyobserver.co.uk/news/local/crawley-girl-13-who-dreams-to-play-football-for-england-meets-world-cup-legend-1-6112060
- ↑ www.itsroundanditswhite.co.uk/2014/04/15/football-for-friendship-are-on-the-hunt-for-talented-young-journalists/
- ↑ https://web.archive.org/web/20140708202936/http:/www.vanluyken.nl/artikel/37-nederlands-voetbaltalent-scoort-tijdens-football-for-friendship-beste-jonge-journalist-uit-nederland-interviewt-franz-beckenbauer-
- ↑ https://web.archive.org/web/20160304111738/http:/www.getbucks.co.uk/news/local-news/12-year-old-bucks-boy-best-young-9095138
- ↑ www.financialexpress.com/india-news/mission-xi-million-picks-chandigarh-girl-ananya-kamboj/689736/
- ↑ https://web.archive.org/web/20150522194216/http:/theindependent.sg/blog/2015/04/27/kids-from-24-countries-in-europe-and-asia-are-celebrating-international-day-of-football-and-friendship/
- ↑ rbth.com/sport/2015/05/15/children_from_24_countries_celebrate_day_of_football_and_friendship_46087.html
- ↑ https://www.theguardian.com/football/2015/apr/26/said-and-done-blatter-putin-david-cameron
- ↑ rbth.com/multimedia/2015/05/12/the-international-day-of-football-and-friendship_95713?crid=325359
- ↑ instagify.com/media/979016253229007447_641360799
- ↑ business-center.amchamchina.org/news/?dir=17&doc=201504262030PR_NEWS_ASPR_____EN90314&andorquestion=OR&&ok=1&passDir=0
- ↑ Super User. "В рамках программы «Футбол для дружбы» учрежден Кубок «Девяти ценностей»". www.joblenobl.ru (kwa Kirusi). Iliwekwa mnamo 2019-04-28.
{{cite web}}
:|author=
has generic name (help) - ↑ www.euronews.com/2017/07/17/f4f-nine-values-cup-2017-goes-to-real-madrid
- ↑ www.dailymail.co.uk/sport/worldcup2014/article-2642473/Vitor-Baia-tips-Portugal-special-World-Cup-Cristiano-Ronaldo-shines-backs-old-boss-Jose-Mourinho-Chelsea.html
- ↑ www.deweekkrant.nl/artikel/2014/mei/27/double_dutchie_dirk_proper_uit_elst_een_voetbal
- ↑ https://web.archive.org/web/20141223203736/http:/bigpicture.ru/?p=516227
- ↑ www.theboltonnews.co.uk/news/11270319.Interview_sends_Megan_Mackey_to_Champions_League_final/
- ↑ sport.rbc.ru/article/172216/
- ↑ en.kremlin.ru/events/president/news/19222
- ↑ www.leparisien.fr/politique/mondial-2014-hollande-invite-deux-clubs-amateurs-a-l-elysee-pour-france-nigeria-28-06-2014-3960541.php
Makala hii kuhusu mambo ya michezo bado ni mbegu. Je, unajua kitu zaidi kuhusu Soka kwa ajili ya Urafiki kama historia yake, uenezi au kanuni zake? Labda unaona katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine habari zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |