Resego Kgosidintsi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Resego Natalie Kgosidintsi[1] ni mwanaharakati wa haki za wanawake na mgombea wa kisiasa kutoka Botswana. Katika shughuli za kisiasa, anajulikana kama Petrol Bomb kwa imani zake za kisiasa zilizo wazi.[2][3][4]

Maisha na Elimu[hariri | hariri chanzo]

Resego Kgosidintsi ni binti wa Bontsibokae na Colline Kgosidintsi,[2] aliyezaliwa kijijini Serowe, Botswana.[1] Akiwa mtoto, alishiriki katika timu zamdahalo wa shule, akisafiri kwenda Ghana na Zimbabwe. Alisoma sayansi ya siasa katika Chuo Kikuu cha Botswana. Alipokuwa chuoni, Kgosidintsi alihudumu kama Waziri wa Habari na Mawasiliano wa Baraza la Wawakilishi wa Wanafunzi, na alikuwa mwenyekiti wa kwanza mwanamke wa Harakati Dhidi ya Kudhibiti Wanafunzi.[2]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. 1.0 1.1 Kgosidintsi, Resego Natalie (2017). "Student Activism and Youth Agency in Botswana". Buwa! (8): 34–40. 
  2. 2.0 2.1 2.2 Kolantsho, Neo. "Resego Unplugged", The Midweek Sun, 2020-11-25. 
  3. Shaya (2022-09-27). "Chillin' out Friday 23 September 2022". TheVoiceBW. 
  4. "Kgosidintsi steers BNFYL". Africa Press (kwa en-US). 2022-05-31. Iliwekwa mnamo 2023-02-24. 
Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Resego Kgosidintsi kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.