Picha ya kiwamba
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Screenshot (pia: kielelezo-skrini) ni picha ya kiwamba au skrini ya kompyuta. Katika Windows ni kazi rahisi kabisa.
Matumizi [hariri]
Inasaidia
- kushika makosa yanayotokea wakati wa kutumia programu za komyuta
- Kunakili picha ambazo hazipatikani kwa njia nyingine
- Mawasiliano na maelewano kati ya watumiaji wa kompyuta wakiwasiliana kwa njia ya barua pepe
Namna ya kufanya picha ya baobonye [hariri]
- Chagua ukurasa au mwandishi au yale unayotaka kuonyesha na hakikisha yameonekana kwenye kiwamba cha komyuta yako
- halafu fungua programu ya picha - kwa mfano "paint" (ama kupitia Start-All Programmes-Acessoires-paint AU kupitia start-execute - mspaint).
- kwenye dirisha unalotaka kuonyesha bofya "print" (kwa kawaida juu upande wa kulia kwenye sehemu ya baobonye). Hutaona badiliko lakini umenakili tayari picha ya skrini yako katika kumbukumbu ya muda.
- Katika paint (au programu nyingine ya picha) tekeleza amri ya "paste" (kwa menu edit-paste AU kwa puku rightclick-paste AU kwa kushika CTRL halafu bofya V).
- Amri hii inaingiza picha ya skrini katika dirisha la paint.
- Picha hii awali bado si imara, unaweza kuisukuma. Bofya "Esc" halafu ni imara.
- Sasa unakata sehemu ile tu ambayo unaitaka kuonyesha halafu unainakili na kuiweka kwa ukurasa mpya ya paint.
- Ukurasa huu unahifadhi kama picha ukichagua format ya jpg.
- Ukihariri picha unaweza pia kuchora duara nyekundu mahali unapotaka kuonyesha hasa.
- Hii faili ya picha unaweza kutuma kwa barua pepe au kuingiza katika wikipedia.
TAHADHARI: Usisahau kubadilisha format kuwa jpg au kile unachotaka kwa sababu pekee yake ni faili kubwa sana ya format ya bmp.