Oyotunji

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kijiji cha Kiafrika cha Oyotunji ni kijiji kilichopo karibu na Sheldon South Carolina na Beaufort County South Carolina kilichoundwa na mtawala Oba Adefunmi Efuntola Oseijeman Adelabu Adefunmi I mwaka 1970.[1][2]

Kijiji cha Oyotunji kimetajwa kutokana na Dola la Oyo, na jina hilo linamaanisha kwa maana halisi Oyo anarudi au Oyo anainuka tena.[1][3] Kijiji cha Oyotunji kina ukubwa wa ekari 27 na kina hekalu la Utamaduni wa Wayoruba ambalo lilisogezwa kutoka Harlem, New York hadi mahali pake pa sasa mwaka 1960.[4][5][6] Katika miaka ya 1970, wakati wa ongezeko kubwa zaidi la watu kijijini, idadi ya wakazi iliongezeka kutoka 5 hadi kati ya 200 na 250. Inasemekana idadi ya watu hupanda na kushuka kati ya familia 5 na 9 kulingana na miaka 10 iliyopita. Awali ilipangwa kuwa katika eneo la Savannah, Georgia, lakini hatimaye ikakaa katika mahali pake pa sasa baada ya mabishano na majirani huko Sheldon kuhusu ngoma na watalii.

Tangu kifo cha Adefunmi mwaka 2005, kijiji kimeongozwa na mwanae, Oba Adejuyigbe Adefunmi II. Kijiji kimejengwa kufanana na vijiji vya mji wa kisasa wa Wayoruba katika Nigeria ya leo, ingawa uimarishaji wa miundombinu ya umma ya kijiji umefanywa chini ya uongozi wa Adefunmi II.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. 1.0 1.1 Peek, Philip M.; Yankah, Kwesi (2004). African Folklore: An Encyclopedia. Routledge. uk. 660. ISBN 9781135948733. OCLC 7385565477. 
  2. Jalloh, Alusine; Falola, Toyin (2008). The United States and West Africa: Interactions and Relations (Rochester studies in African history and the diaspora) 34. University Rochester Press. uk. 32. ISBN 9781580463089. OCLC 166379802. 
  3. Hunt, Carl M. (1979). yotunji Village: the Yoruba movement in America. University Press of America (University of Michigan). ISBN 9780819107480. OCLC 5625761. 
  4. Curry, Mary Cuthrell (1997). Making the Gods in New York (The Yoruba Religion in the African American Community). Taylor & Francis, Garland series (Studies in African American history and culture). uk. 7. ISBN 9780815329190. OCLC 925262399. 
  5. Murphy, Larry G (2000). Down by the Riverside: Readings in African American Religion (Religion, Race, and Ethnicity). NYU Press. uk. 257. ISBN 9780814755808. OCLC 44727724. 
  6. Kail, Tony M. (2008). Magico-Religious Groups and Ritualistic Activities: A Guide for First Responders. CRC Press. ku. 41–42. ISBN 9781420051872. OCLC 941224974.