Nungunungu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Nungunungu/ Nungu
MainePorcupine.JPG
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Mammalia (Wanyama wenye viwele wanaonyonyesha wadogo wao)
Oda: Rodentia
Familia: Hystricidae

Erethizontidae

Jenasi: Hystricidae

Atherurus
Hystrix
Trichys
Erethizontidae
Chaetomys
Coendou
Echinoprocta
Erethizon
Sphiggurus

Nungnungu ni wanyama wagugunaji wenye ngozi yenye miiba iliyochongoka wanayotumia kujilinda na maadui. Walienea katika ulimwengu wa sasa na ulimwengu wa zamani. Katika wanyama wagugunaji ni watatu kwa ukubwa, wakitanguliwa na capybara na buku. Nungu wana urefu kati ya sm 20 - 25. Uzito wao wakaribia kg 5.4 - 16. Wana umbo la duara, wakubwa na wataratibu kweli. Nungu hawa katika rangi mbalimbali ya kijivu, na mara chache nyeupe. Kujihami kwa miba kwa nungu hufanana na kule kwa kalunguyeye (Erinaceomorpha) na ekidna (Monotremata).

Spishi[hariri | hariri chanzo]

Nungu wa Dunia ya Kale

Nungu ni miongoni mwa spishi 27 za wanyama wagugunaji (rodent) wa familia ya Erethizontidae au Hystricidae. Nungu wanatofautiana kwa ukubwa. Nungu aitwaye Rothschild's Porcupine wa Amerika ya kusini ana uzito pungufu ya nusu kilo ; wa Afrika anaweza kukua mpaka kufika kufikia kilo 10. Familia mbili hizi za nungu ni tofauti kabisa na ingawa wote wapo kwenye tawi la Hystricognathi wa oda ya Rodentia, hawa husiani sana. Nungu kumi na moja wa Dunia ya kale, wengi walikuwa ni wa nchi kavu huku wakiwa wakubwa kidogo na wana miba iliyojikusanya kwa makundi. Inaaminika kuwa wametokana na hystricognaths wengine takribani miaka milioni 30 iliyopita mapema zaidi kuliko nungunungu wa dunia ya leo.

Nungu wa dunia ya leo wanaumbo ndogo mafi (japokuwa nungu wa Amerika ya Kaskazini wanafikia kama sm 85 kwa maelfu na uzito wa kilogramu 18), huku miiba yao ikiwa imejishikiza mmoja mmoja badala ya kwa makundi na ni wakweaji wazuri,na hutumia muda wao mwingi juu ya miti.Nungu wa dunia ya leo miiba yao ilijitokeza na kukua kwa kujitegemea baadae na wanahusiana zaidi na familia nyingine za rodent kuliko namna wanavyofahamiana na nungu wa dunia ya kale. Nungu kwa wastani wana uwezo wa kuishi muda mrefu na wanashikilia rekodi miongoni mwa familia yao ya rodent kwa kuishi kwa kiasi cha muda mrefu zaidi.[1] ambayo imevujwa hili karibuni na panya aina ya Naked Mole Rat (Heterocephalus glaber).

Miiba[hariri | hariri chanzo]

Miba ya nungu huchukua sura mbalimbali kulingana na spishi, lakini yote ni nywele zilizo boreshwa na kufunikwa na keratini.na zimejishikiza kwenye misuli ya ngozi. Nungu wa kale (Hystricidae) wana miiba iliyojikusanya kwenye makundi huku kwa nungu wa dunia ya mpya (Erethizontidae), miiba, mmojammoja, imechanganyika na na ufumele, manyoya ya chini na nywele, Miba huachiwa kwa kuigusa, au hudondoka pale ambapo nungu anajitikisa, lakini hawezi kamwe kurushwa kwa adui, pamoja na imani iliozoeleka. Miba mipya hukua huchukua nafasi ya ile iliyopotea.

Makazi[hariri | hariri chanzo]

Nungu hupatikana sana katika maeneo ya kawaida na tropiki ya Asia, Italia, Afrika na Amerika ya Kusini na Kaskazini. Nungu huishi kwenye misitu, jangwani sehemu zenye miamba, vilima na nyikani. Baadhi ya nungu wa Dunia Mpya huishi kwenye miti, lakini nungu wa Dunia wa Kale wanakaa ardhini. Nungu huweza kupatikana hata kwenye miamba kwenye ardhi yenye hata urefu wa mita 3700. Nungu ni wanyama wa usiku.

Ulambaji chumvi[hariri | hariri chanzo]

Nungu anapotafuta chumvi wakati mwengine huweza kupata kupitia makazi ya watu na kwa tabaka za mbao zilizopakwa sodium naitreti, [2] rangi za kuta, mishikio ya vifaa,viatu, nguo na vitu vingine vilivyopata jasho. Nungu pia huvutiwa na barabara ambazo chumvi hutumika kuyeyushia barabafu, na mara kadhaa huonekana wakilamba magurudumu ya gari zilizopita kwenye barabara hizo. Chumvi maalumu iliyotengwa kama inaweza kuwasaidia wasijiumize. Vyanzo asili vya chumvi ambavyo nungu hutumia hujumuisha mimea yenye chumvi, mifupa ya wanyama, magamba ya miti, matope kwenye udongo wenye chumvi sana, na vitu vilivyo shikwa na mkojo.

Imani potofu[hariri | hariri chanzo]

Kwa kipindi kirefu nungu huaminika kuwa wanauwezo wa kurusha miiba yao kwa adui, hii imekanushwa vikali, baada ya kufahamu kuwa miba hulegea na kuanguka yanyewe.
Nungu wameanza kufugwa Kenya na wanatumika kama kinweo kwa uzuri kabisa

Uanishaji[hariri | hariri chanzo]

Nungu wa Amerika ya kaskazini akitafuta chakula kwenye nyasi

Spishi za Afrika[hariri | hariri chanzo]

Spishi za mabara mengine[hariri | hariri chanzo]

 • Hystricidae (Nungunungu wa Dunia ya Kale)
  • Asiatic Brush-tailed Porcupine, Atherurus macrourus
  • Himalayan Porcupine, Hystrix hodgsoni
  • Indian Porcupine, Hystrix indicus
  • Malayan Porcupine, Hystrix brachyura
  • Sunda Porcupine, Hystrix javanica
  • Sumatran Porcupine, Hystrix sumatrae
  • Bornean Porcupine, Thecurus crassispinis
  • Philippine Porcupine, Thecurus pumilis
  • Long-tailed Porcupine, Trichys fasciculata
 • Erethizontidae (Nungunugnu wa Dunia Mpya)
  • Brazilian Porcupine, Coendou prehensilis
  • Bicolor-spined Porcupine, Coendou bicolor
  • Rothschild's Porcupine, Coendou rothschildi
  • Mexican Tree Porcupine, Sphiggurus mexicanus
  • South American Tree Porcupine, Sphiggurus spinosus
  • Bahia Hairy Dwarf Porcupine, Sphiggurus insidiosus
  • Pallid Hairy Dwarf Porcupine, Sphiggurus pallidus (spishi isiyokubalika)
  • Brown Hairy Dwarf Porcupine, Sphiggurus vestitus
  • Orange-spined Hairy Dwarf Porcupine, Sphiggurus villosus
  • Stump-tailed Porcupine, Echinoprocta rufescens
  • Bristle-spined Porcupine, Chaetomys subspinosus (wakati mwingine huonwa kama katika Echimyidae)