Mkoa wa Taoudenit

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Maeneo ya Taoudenit (nyekundu)
Ramani hii inaonyesha Taoudenit kama sehemu ya Mkoa wa Timbuktu

Taoudénit (kwa Kibambara: Taudeni Dineja) ni mkoa wa Mali ulioundwa kisheria mwaka wa 2012 kutoka sehemu ya kaskazini ya Mkoa wa Timbuktu. [1] [2]

Utekelezaji halisi wa uanzishwaji wa mkoa huo ulianza tarehe 19 Januari 2016 kwa kumteua Abdoulaye Alkadi kuwa gavana wa eneo hilo. [3] Wajumbe wa baraza la mpito la mkoa waliteuliwa tarehe 14 Oktoba 2016. [4] Jenerali Abderrahmane Ould Meydou alichukua nafasi ya Alkadi kama gavana mnamo Julai 2017. [5]

Mkoa umegawanywa katika wilaya (cercles) sita: Achouratt, Al-Ourche, Araouane, Boudje-Beha, Foum-Alba na Taoudenit. [6] Makao makuu yanapangwa kuwa Taoudenit, [6] ingawa serikali kwa sasa iko Timbuktu kutokana na ukosefu wa miundombinu huko Taoudenit [7], pamoja na hali tata ya usalama.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "LOI No 2012-017 DU 02 MARS 2012 PORTANT CREATION DE CIRCONSCRIPTIONS ADMINISTRATIVES EN REPUBLIQUE DU MALI". Journal officiel de la République du Mali. 2 March 2012. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-11-23. Iliwekwa mnamo 21 February 2017.  Check date values in: |date=, |accessdate= (help)
  2. "Report of the Secretary-General on the situation in Mali". MINUSMA. 28 March 2016. Iliwekwa mnamo 21 February 2017.  Check date values in: |date=, |accessdate= (help)
  3. "Régionalisation: Deux Nouvelles régions créées au Mali". Malijet. 21 January 2016. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-02-22. Iliwekwa mnamo 21 February 2017.  Check date values in: |date=, |accessdate= (help)
  4. Report of the Secretary-General on the situation in Mali, Tovuti ya Minusma tar. 30.12.2016
  5. "Taoudenit : Le général Ould Meydou installé dans ses fonctions de gouverneur de région". Malizine. 22 July 2017. Iliwekwa mnamo 18 October 2018.  Check date values in: |date=, |accessdate= (help)
  6. 6.0 6.1 "Mali : Taoudeni, contrée historique". 21 February 2017. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2022-01-10. Iliwekwa mnamo 25 May 2017.  Check date values in: |date=, |accessdate= (help)
  7. "Report of the Secretary-General on the situation in Mali". MINUSMA. 30 December 2016. Iliwekwa mnamo 21 February 2017.  Check date values in: |date=, |accessdate= (help)"Report of the Secretary-General on the situation in Mali" (PDF). MINUSMA. 30 December 2016. Retrieved 21 February 2017.