Maktaba ya IOGT
Mandhari
Maktaba ya IOGT nchini Tanzania iko chini ya shirika lisilo la kiserikali linalojishughulisha na uzuiaji wa matumizi ya dawa za kulevya, hasa kwa vijana. Maktaba hii inakusanya na kuhifadhi habari mbalimbali kutoka ndani ya nchi na hata nchi jirani za Afrika Mashariki, Ulaya, Asia na Amerika.
Habari hizi ziko katika mifumo mbalimbali kama kanda za video, majarida, vitabu na vipeperushi. Watu wa aina zote, umri na kiwango chochote cha elimu wanakaribishwa kutumia maktaba hii. Maktaba ina nafasi ya kusomea kwa wasomaji wanne mpaka sita kwa wakati mmoja. Kuna kiyoyozi, televisheni na mtandao kwa watumiaji.
Ofisi za IOGT ipo karibu na hospitali ya Muhimbili, Dar es Salaam.