Majadiliano:Vielezi

Yaliyomo ya ukurasa hayatumiki katika lugha nyingine.
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Vielezi ni maneno yanayoelezea tendo lilivyofanyika au litakavyofanyika.Vielezi hufafanua kitendo kilitendeka wapi,vipi,mara ngapi na namna gani.

Aina za vielezi[hariri chanzo]

Kuna aina nne 4 za vielezi.aina hizo ni:

  • (i)Vielezi vya namna au jinsi
  • (ii)Vielezi vya mahali
  • (iii)Vielezi vya idadi
  • (iv)Vielezi vya wakati

(i)Vielezi vya namna au jinsi[hariri chanzo]

Ni aina ya vielezi ambavyo huelezea namna au jinsi ya kutendeka kwa tendo. Vielezi hivi huelezea jinsi gani tendo hilo limetendeka.

(ii)Vielezi vya mahali[hariri chanzo]

Ni aina ya vielezi ambavyo huelezea mahali kulikotendeka tendo.Vielezi hivi hueleza tendo hilo limetendeka wapi.

(iii)Vielezi vya idadi[hariri chanzo]

Ni aina ya vielezi ambavyo huelezea idadi ya kutendeka kwa tendo.Vielezi hivi hueleza tendo hilo limetendeka mara ngapi.

(iv)Vielezi vya wakati[hariri chanzo]

ni aina ya vielezi ambavyo hueleza wakati wa kutendeka kwa tendo.Vielezi hivi hueleza ni lini hasa tendo hili limetendeka.