Majadiliano:Utegili (fizikia)

Yaliyomo ya ukurasa hayatumiki katika lugha nyingine.
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Utegili kutoka neno plasma la kiingereza ! leza kutoka Laser yaani kifupi cha Light Amplification By Stimulation of the Electromagnetic Radiation.

Kiswahili tuseme: Ukuzaji wa Nuru kwa Uchochezi wa Mnururisho wa Uga Usumaku Umeme... UNUMUU, ha?

Kuna neno napenda kutumia la kiswahili, BIRU...

Basi Leza=Biru

Nimeongeza "plasma" baada ya "utegili" pamoja na redirect yake. Hali halisi maneno yanayotumiwa katika lugha za nje yaingizwa mara nyingi katika matumizi ya Kiswahili hata kama kuna neno lililopendekezwa na TUKI au taasisi nyengine za lugha kama vile "utegili" kwa mfano wetu. Ila tu "plasma" si Kiingereza; ni neno la Kigiriki yaani neno la kisayansi linalotumiwa katika lugha nyingi. Kwa kawaida ushauri wetu ni tufuate kamusi ya KAST isipokuwa ni muhimu kuongeza na kuunganiosha maneno mengine hata yasipopendwa na wataalamu ili watu wengi wapate kutumia kamusi yetu ya wikipedia. --Kipala 16:39, 13 Juni 2007 (UTC)[jibu]