Lango:Kenya/Wasifu uliochaguliwa/3

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Mwai Kibaki ni rais wa tatu wa Jamhuri ya Kenya akiwa ametanguliwa na Rais wa Kwanza wa Kenya,Mzee Jomo Kenyatta, na Daniel Arap Moi. Jina lake la kubatizwa ni Emilio Stanley.

Kibaki alisoma uchumi, historia na sayansi ya siasa katika chuo kikuu cha Makerere, Kampala, Uganda. Akiwa mwanafunzi Makerere, Kibaki alikuwa ni mwenyekiti wa chama cha wanafunzi toka Kenya, Kenya Students' Association. Alipomaliza masomo yake mwaka 1955 alipewa tuzo kutokana na kufanya vyema katika mitihani. Tuzo hiyo ilimwezesha kwenda kusoma katika chuo cha London School of Economics. Alipomaliza masomo alikwenda kufundisha katika chuo kikuu cha Makerere. Baadaye aliacha kazi ya kufundisha na kuwa mtendaji mkuu wa chama cha Kenya African National Union.

(Soma Zaidi...)