Nenda kwa yaliyomo

Kiteso

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Kiteso (lugha))

Kiteso (pia inajulikana kama Iteso au Ateso) ni lugha ya Kinilo-Sahara, inayozungumzwa na kabila ya Wateso nchini Uganda na Kenya. Ni mmojawapo wa nguzo ya lugha za Kiteso-Kiturkana.

Katika sensa ya watu ya mwaka wa 1991 idadi ya watu karibu 999,537 ilikuwa inazungumza lugha ya Kiteso kote nchini Uganda. Watu ambao idadi yao iliwastaniwa kuwa laki 279 nchini Kenya pia waliizungumza lugha hii. Kodi yake ya SIL ni TEO.[1]

Asili ya Lugha ya Kiteso ni eneo linaloitwa Teso.

Lugha ya kawaida

[hariri | hariri chanzo]

Habari --- yoga
U hali gani? --- Ijai biai (umoja) Ijaasi biai (wingi)
Salama salmini, na wewe je? Ejokuna, arai ijo?
Njema --- ejokuna
Waitwaje? --- Ingai bo ekon'kiror?
Jina langu ni ... --- Eka'kiror ...
Jina --- Ekiror
Ni vizuri kukujua. --- Eyalama ewanyun (pia: Eyalama aanyun)
Tutaonana baadaye tena --- Awanyunos Bobo
Kitabu --- Eitabo
Sababu --- Naarai

Sentensi ya kwanza katika Biblia inaweza kutafsiriwa kama Ageunet, abu Edeke Kosub akwap had akuju (kwa Kiswahili: "Mwanzoni Mungu aliumba dunia na mbingu").

Kama lugha zingine nyingi, Kiteso pia ina majina ya jinsia. Katika maneno ya lugha ya Kiteso, jinsia huashiriwa kwa kawaida katika herufi ya kwanza ya neno. Ikiwa herufi E au herufi O ni herufi ya kwanza katika jina basi jina hilo ni la kiume. Ikiwa herufi A ni herufi ya kwanza katika jina basi jina hilo ni la

Mwanaume wa Kiteso anaweza kujiita Etesot na mwanamke anaweza kujiita Atesot

Jimbi au jogoo ukipenda anajulikana kwa lugha ya Kiteso kama "Ekokor " na kuku anajulikana kama "Akokor ".

Kama lugha zingine ambazo zina majina ya kijinsia, mambo ambayo kwa kawaida hayawezi kuwekwa katika jamii ya kijinsia bado yanaweza kuwekwa kwa jamii kimakusudi. Mfano moja wa mambo au maneno haya ni "Etogo " ambayo inamaanisha nyumba kwa lugha ya Kiteso na hospitali inaitwa "Adekis ". Shati inajulikana kama "Esaati ".

Neno "Akwii " linamaanisha majani, hata hivyo kulitamka neno hilo kwa msongo uliorefushwa mwishoni kunaibadilisha neno hilo kuwa jina la mwanamke. Kubadilisha jina hilo kuwa "Okwii " hubadilisha neno hilo kuwa jina la mwanaume.

Wakati wa kuhesabu katika lugha ya Kiteso, idadi ya 6 hutafsiriwa kama 5 +1, 7 ni 5 +2 na kadhalika. Katika mtindo huo 16 ni 10 +5 +1, 17 ni 10 +5 +2. 21 tena ni 20 +1, 26 pia ni 20 +5 +1. Hakuna neno katika lugha ya Kiteso inayoashiria idadi kubwa isiyojulikana. Neno sufuri ni Enooti .

  1. Idiopet au Ipe
  2. Iyarei
  3. Iuni
  4. Iwongon
  5. Ikanyi
  6. Ikanyikadiop au Ikanyikape
  7. Ikanyikaare
  8. Ikanyilauni
  9. Ikanyikawongon
  10. Itomon
  11. Itomonkadiop au Itomonkape
  12. Itomonkaarei
  13. Itomonkauni
  14. Itomonkawongon
  15. Itomonkakany
  16. Itomonkakanyikaape
  17. Itomonkakanyikaarei
  18. Itomonkakanyikauni
  19. Itomonkakanyikawongon
  20. Akaisaarei
  21. Akaisaareikayediopet
  22. Akaisaareikakanuyarei
  23. Akaisaareikakanuiuni

Idadi kubwa ni kama ifuatavyo: --

Idadi idadi ya Kiteso katika maneno
[45] Akaisauni
40 Akaisaagon
50 Akaisakany
60 Akaisakanyikaape
60 Akaisakanyikaape
70 Akaisakanyikaarei
80 Akaisakanyikauni
[75] Akaisakanyikawogon
100 Akwatat
101 Akwatatkidiopet

| |)

Maneno yaliyokopwa

[hariri | hariri chanzo]

Lugha ya Kiteso imekopa idadi ya maneno, kimsingi kutoka Kilatini, ambayo baadaye ilikwenda kutumika katika lugha ya Kiingereza, hivyo basi mfanano.

  • Herufi E katika maneno ya Kiteso hutamkwa kama É au "ay".

Maneno yenye alama ya asteriski (*) huonyesha kwamba herufi ya mwisho katika neno hilo la Kiteso ni kimya.

Neno la Kiswahili Neno la Kiteso
Gari Emotoka
Runinga Etelevision
Radio Eredio
Mashine ya Fax Afakis mashin
Barua Pepe E-emeilo *
Intaneti E-Intanet
Tarakilishi Akompuita
Simu Etelefoni *
Kicheza Rekodi A rekod puleya
Kicheza CD A Sidi puleya
Kicheza DVD Adividi puleya
Diski Adisiki *
  1. http://www.ethnologue.com/language/teo Accessed 2007/07/09

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]