Kidonda cha duodenamu
Kidonda cha duodenamu | |
---|---|
Mwainisho na taarifa za nje | |
Kundi Maalumu | Gastro-enterolojia |
ICD-10 | K25.–K27. |
ICD-9 | 531–534 |
DiseasesDB | 9819 |
MedlinePlus | 000206 |
eMedicine | med/1776 ped/2341 |
MeSH | D010437 |
Ugonjwa wa kidonda cha duodenamu (UKD), huitwao kwa kawaida kidonda cha tumbo, ni mpasuko katika sehemu ya juu ya tumbo, sehemu ya kwanza ya utumbo mdogo, au mara chache umio.[1][2] Kidonda tumboni huitwa kidonda cha tumbo huku kile kilicho kwenye sehemu ya kwanza ya matumbo kikiitwa kidonda cha duodenamu. Dalili ya kawaida sana ni kuamka usiku ukiwa na maumivu ya fumbatio la juu au maumivu ya fumbatio la juu ambayo hupungua unapokula. Maumivu haya mara nyingi huelezwa kuwa maumivu yayanayochoma au yasiyo kali. Dalili zingine hujumuisha kupiga mbweu., kutapika, kupungukiwa na uzani, au kutokuwa na hamu ya kula. Takribani thuluthi ya watu walio wazee zaidi hawawi na dalili.[1] Matatizo yanaweza kujumuisha kuvuja damu, kutoboka, na kuzibika kwa tumbo. Uvujaji damu hutokea kwa asilimia 15 ya watu.[3]
Kisababishi na utambuzi
[hariri | hariri chanzo]Visababishi vya kawaida hujumuisha bakteria, Filori helikobakta na dawa ya kumaliza inflamesheni isiyo na steroidi (NSAIDs).[1] Visababishi vingine visivyo vya kawaida hujumuisha uvutaji tobako, mfadhaiko unaotokana na ugonjwa kali, Ugonjwa wa beseti, Sindromu ya ollinger-Ellison, Ugonjwa wa kroni na sirosisi ya maini, kati ya zingine.[1][4] Watu waliozeeka zaidi huathirika zaidi na athari za NSAIDs. zinazosababisha kidonda Kwa kawaida utambuzi ukadiriwa kwa sababu ya dalili zinazodhihirika zinazodhibitishwa kwa endoskopi au barium swallow. Filori H. inaweza kutambuliwa kwa kufanya uchunguzi wa damu kutambua iwapo inakingamwili, uchunguzi wa pumzi wa urea, kuchunguza kinyesi ili kutambua dalili za bakteria au biopsi ya tumbo. Hali zingine zinazosababisha dalili sawa hujumuisha saratani ya tumbo, ugonjwa wa moyo wa koronari, na inflamesheni ya sehemu ya juu ya tumbo au kibofu cha nyongo.[1]
Uzuiaji na matibabu
[hariri | hariri chanzo]Lishe haichangii sana katika kusababisha au kuzuia vidonda.[5] Matibabu hujumuisha kutovuta sigara, kutotumiaNSAIDs, kutokunywa pombe, na dawa za kupunguza asidi ya tumbo. Kwa kawaida dawa inayotumika kupunguza asidi kwa kawaida ni proton pump inhibitor (PPI) au H2 blocker huku matibabu ya wiki nne yakipendekezwa hapo mwanzo.[1] Vidonda vinavyosababishwa na filori H. hutibiwa kwa mchanganyiko wa dawa kama vile amoxicillin, clarithromycin, naPPI. Ukinzani wa antibiotikinti unazidi kuongezeka na hivyo matibabu yanaweza kutosaidia kila wakati.[6] Vidonda vinavyovuja damu vinaweza kutibiwa kwa endoskopi, kwa upasuaji wa wazi unaotumika tu kwa kawaida pale ambapo haijafaulu.[3]
Epidemolojia na historia
[hariri | hariri chanzo]Vidonda vya tumbo hupatikana katika takribani asilimia 4 ya watu.[1] Takribani asilimia 10 ya watu hupata kidonda cha tumbo katika wakati fulani maishani mwao.[7] Vilisababisha vifo 301,000 katika mwaka wa 2013 idadi iliyopungua kutoka kwa vifo 327,000 katika mwaka wa 1990.[8] Maelezo ya kwanza ya kidonda cha peptisi kilichotobokayalikuwa katika mwaka wa 1670 katika Princess Henrietta ya Uingereza.[3] filori H. iligunduliwa kwanza katika mwaka wa 1981 na Barry Marshall na Robin Warren.[6]
Marejeleo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ 1.0 1.1 1.2 1.3 1.4 1.5 1.6 Najm, WI (Septemba 2011). "Peptic ulcer disease". Primary care. 38 (3): 383–94, vii. PMID 21872087.
{{cite journal}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Definition and Facts for Peptic Ulcer Disease". http://www.niddk.nih.gov/. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2015-04-02. Iliwekwa mnamo 28 Februari 2015.
{{cite web}}
: External link in
(help); Unknown parameter|website=
|=
ignored (help)CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ 3.0 3.1 3.2 Milosavljevic, T; Kostić-Milosavljević, M; Jovanović, I; Krstić, M (2011). "Complications of peptic ulcer disease". Digestive diseases (Basel, Switzerland). 29 (5): 491–3. PMID 22095016.
- ↑ Steinberg, KP (Juni 2002). "Stress-related mucosal disease in the critically ill patient: risk factors and strategies to prevent stress-related bleeding in the intensive care unit". Critical care medicine. 30 (6 Suppl): S362-4. PMID 12072662.
{{cite journal}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Eating, Diet, and Nutrition for Peptic Ulcer Disease". http://www.niddk.nih.gov. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2015-03-20. Iliwekwa mnamo 28 Februari 2015.
{{cite web}}
: External link in
(help); Unknown parameter|website=
|=
ignored (help)CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ 6.0 6.1 Wang, AY; Peura, DA (Oktoba 2011). "The prevalence and incidence of Helicobacter pylori-associated peptic ulcer disease and upper gastrointestinal bleeding throughout the world". Gastrointestinal endoscopy clinics of North America. 21 (4): 613–35. PMID 21944414.
{{cite journal}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Snowden FM (Oktoba 2008). "Emerging and reemerging diseases: a historical perspective". Immunol. Rev. 225 (1): 9–26. doi:10.1111/j.1600-065X.2008.00677.x. PMID 18837773.
{{cite journal}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ GBD 2013 Mortality and Causes of Death, Collaborators (17 Desemba 2014). "Global, regional, and national age-sex specific all-cause and cause-specific mortality for 240 causes of death, 1990-2013: a systematic analysis for the Global Burden of Disease Study 2013". Lancet. doi:10.1016/S0140-6736(14)61682-2. PMID 25530442.
{{cite journal}}
:|first1=
has generic name (help)CS1 maint: date auto-translated (link) CS1 maint: numeric names: authors list (link)