Homa ya Bonde la Ufa
Rift Valley fever | |
---|---|
Mwainisho na taarifa za nje | |
Kundi Maalumu | Infectious diseases, veterinary medicine |
ICD-10 | A92.4 |
ICD-9 | 066.3 |
DiseasesDB | 31094 |
MeSH | D012295 |
Homa ya Bonde la Ufa (RVF) ni ugonjwa wa virusi ambao unaweza kusababisha dalili ndogo hadi kuu. Dalili ndogo zinaweza kujumuisha: homa, maumivu ya misuli, na maumivu ya kichwa ambayo mara nyingi hudumu hata kwa wiki moja. Dalili kali zinaweza kujumuisha: kupoteza uwezo wa kuona kuanzia wiki tatu baada ya kuambukizwa, maambukizi ya ubongo husababisha maumivu makali ya kichwa na kuchanganyikiwa, na kuvuja damu pamoja na matatizo ya ini yanayoweza kutokea siku chache baada ya kuambukizwa. Watu wanaovuja damu wana uwezekano wa kufa wa hata 50%.[1]
Kisababishi
[hariri | hariri chanzo]Ugonjwa huu husababishwa na virusi, vya RVF vya aina ya Phlebovirus. Ugonjwa huu husambazwa kwa kuguza damu ya wanyama walioambukizwa, kupumua hewa ya eneo kuchinjia mnyama, kunywa maziwa mabichi ya mnyama aliyeambukizwa, au kuumwa na mbu walioambukizwa. Mifugo kama vile ng’ombe, kondooo, mbuzi, na ngamia wanaweza kuathiriwa. Ugonjwa huu mara nyingi husambazwa katika mifugo hawa kupitia mbu. Si dhahiri kwamba binadamu anaweza kumwambukiza mwingine. Utambuzi hufanywa kwa kutafuta antibodi za kukabiliana na virusi au uwepo wa virusi vyenyewe katika damu.[1]
Kinga na Matibabu
[hariri | hariri chanzo]Kinga ya ugonjwa huu katika binadamu ni kwa kuwachanja wanyama dhidi ya ugonjwa wenyewe. Chanjo lazima ifanywe kabla ya mzuko kwa sababu ikifanywa wakati wa mzuko inaweza kuzorotesha hali hii. Kuzuia kuhama kwa wanyama wakati wa mzuko pia kunaweza kusaidia. Kupunguza idadi ya mbu na kujikinga dhidi ya kuumwa nao pia husaidia. Kuna chanjo ya binadamu; hata hivyo, kufikia mwaka wa 2010, chanjo hii haipatikani katika sehemu nyingi. Hakuna tiba maalum baada ya kuambukizwa.[1]
Epidemiolojia na historia
[hariri | hariri chanzo]mizuko ya ugonjwa huu imetokea barani Afrika na Arabia pekee. Mizuko kwa kawaida hutokea katika misimu ya mvua nyingi inayosababisha ongezeko la idadi ya mbu.[1] Ugonjwa huu uliripotiwa mara ya kwanza katika mifugo katika Bonde la Ufa la Kenya miaka ya kwanza ya 1900,[2] navyo virusi vyake vilitambuliwa kwa mara ya kwanza mwaka wa 1931.[1]
References
[hariri | hariri chanzo]- ↑ 1.0 1.1 1.2 1.3 1.4 "Rift Valley fever". Fact sheet N°207. World Health Organization. Mei 2010. Iliwekwa mnamo 21 Machi 2014.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Palmer, S. R. (2011). Oxford textbook of zoonoses : biology, clinical practice, and public health control (tol. la 2nd). Oxford u.a.: Oxford Univ. Press. uk. 423. ISBN 9780198570028.