Hidrokaboni
Hidrokaboni ni aina mbalimbali za kampaundi ogania za kikemia zinazojengwa kwa atomi za hidrojeni na kaboni pekee.
Kiasili zinapatika hasa katika mafuta ya petroliamu iliyotokea kutokana na mchakato wa kuoza kwa mimea na mata ogania yenye kaboni na hidrojeni nyingi. Hidrokaboni haziwezi kuingia katika mmenyuko wa kikemia na maji.
Hidrokaboni ni chanzo muhimu cha nishati kwa binadamu duniani; petroli na diseli ni mchanganyiko wa aina za hidrokaboni.
Yaliyomo |
Vikundi vya hidrokaboni[hariri]
Hidrokaboni hupangwa katika vikundi 5.
Alkani[hariri]
Alkani ni hidrokaboni za kimsingi. Fomula yao ni CnH2n+2.
| Jina la alkani | Fomula |
|---|---|
| Methani | CH4 |
| Ethani | C2H6 |
| Propani | C3H8 |
| Butani | C4H10 |
| Pentani | C5H12 |
| Hexani | C6H14 |
| Heptani | C7H16 |
| Oktani | C8H18 |
| Nonani | C9H20 |
| Decane | C10H22 |
Alkeni[hariri]
Alkeni hufanana na alkani. Lakini zina muungo jozi kati ya kaboni na kaboni. Fomula yao ni CnH2n.
| Jina la alkeni | Fomula |
|---|---|
| Etheni | C2H4 |
| Propeni | C3H6 |
| Buteni | C4H8 |
| Penteni | C5H10 |
| Hexeni | C6H12 |
| Hepteni | C7H14 |
| Okteni | C8H16 |
| Noneni | C9H18 |
| Deseni | C10H20 |
Alkini[hariri]
Alkynes have a carbon to carbon triple bond. CnH2n-2 is their general formula.
| Alkyne Name | Formula |
|---|---|
| Ethyne | C2H2 |
| Propyne | C3H4 |
| Butyne | C4H6 |
| Pentyne | C5H8 |
| Hexyne | C6H10 |
| Heptyne | C7H12 |
| Octyne | C8H14 |
| Nonyne | C9H16 |
| Decyne | C10H18 |
Sikloalkani[hariri]
Sikloalkani ni isomeri za alkeni. Fomula yao ni pia (CnH2n) lakini hazina muungo jozi kati ya kaboni na kaboni.
| Jina la Sikloalkani | Fomula |
|---|---|
| Siklopropani | C3H6 |
| Siklobutani | C4H8 |
| Siklopentani | C5H10 |
| Siklohexani | C6H12 |
| Sikloheptani | C7H14 |
| Sikloctani | C8H16 |
| Siklononani | C9H18 |
| Siklodekani | C10H20 |
Alkadini[hariri]
Alkadini zina muungo jozi mbili kati ya kaboni na kaboni. Fomula ni CnH2n-2. Hizi ni isomeri za Alkini.
Hidrokaboni aromatiki[hariri]
Hidrokaboni aromatiki ni molekuli ogania yenye umbo la mviringo tambarare. Fomula yao ni CnH2n-6 na "n" ni sawa na kubwa kubwa kuliko 6.