Haidra (mnyama)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Haidra
Haidra kijani (Hydra viridissima)
Haidra kijani (Hydra viridissima)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia
Nusuhimaya: Eumetazoa
Faila: Cnidaria (Wanyama-upupu)
Nusufaila: Medusozoa (Wanyama kama konyeza)
Ngeli: Hydrozoa (Wanyama kama haidra)
Oda: Anthoathecata
Nusuoda: Aplanulata
Familia: Hydridae (Haidra)
Jenasi: Hydra
Spishi: 40, angalia makala

Haidra au hidra (kutoka Kigiriki Ὕδρα, hyudra, "wa majini", kupitia Kiingereza hydra) ni wanyama wasio na uti, mwenye tabaka mbili za seli za mwili. Wanaishi katika maji safi. Mwili wao ni kama mwale. Wana kama mfuko katika miili yao ambayo hutumika kwa wote kuchukua chakula na kuondosha taka.

Haidra ni wanyama-upupu (oda Cnidaria) walio na seli za kupigia kwenye minyiri yao. Haidra ni wadogo kiumbo (hadi mm 10). Haidra wananaweza kupatikana katika sehemu yoyote ya maji ambayo hayajachafuka.

Utafiti wa hivi karibuni umegundua kwamba huzalisha protini iitwayo haidramasini na inayokinga dhidi ya vijidudu.

Inaonekana kuwa hawazeeki wala kufa kwa sababu ya uzee.

Picha[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Haidra (mnyama) kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.