Djibril Diallo
Mandhari
Dakta Djibril Diallo ni mzaliwa wa Senegal. Amewahi kuwa mkurugenzi wa mawasiliano wa Shirika la Maendeleo ya Viwanda la Umoja wa Mataifa, mshauri maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusiana na mkutano wa kimataifa wa haki za binadamu. Tena alikuwa waziri nchini Mali.
Hivi sasa anahudumia ofisi ya Umoja ya Mataifa inayojihusisha na miradi ya kuleta amani kwa kutumia michezo. Diallo pia ni msemaji wa Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.