Chamkano

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Machamkano ya nusu na robo kwa mfano wa keki

Chamkano (ing. Archived 24 Machi 2015 at the Wayback Machine. fraction) ni namna ya kutaja sehemu sawa za jumla fulani katika lugha ya hisabati.

Mifano ya machamkano katika maisha ya kawaida ni nusu, theluthi, robo. Tunaweza kutaja theluthi mbili, robo mbili ambayo ni sawa na nusu au robo tatu.

Chamkano huandikwa kwa tarakimu ya kuhesabu inayoandikwa juu ya mstari na tarakimu za kutaja idadi ya sehemu zinazoandikwa chini ya mstari:

  • au 1/2 = nusu moja
  • au 3/4 = robo tatu
  • au 17/3 = kumi na saba theluthi
  • au 10/12 = kumi za kumi na mbili