Bard (roboti mazungumzo)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Nembo ya Bard, roboti mazungumzo kutoka Google


Bard ni roboti la mazungumzo linalotumia akili bandia ya kuzalisha lililotengenezwa na Google. Mwanzoni lilijengwa juu ya LaMDA, familia ya mifumo mikubwa ya lugha (MMLs), baadae liliboreshwa na kutumia PaLM kabla halijaboreshwa tena na kutumia Gemini. Bard iliundwa na kutolewa Machi 2023, kujibu ujio wa kishindo wa ChatGPT, roboti lingine la mazungumzo kutoka OpenAI.

OpenAI waliizindua ChatGPT mnamo Nevemba 2022, mafanikio na umaarufu uliyopata ChatGPT uliwashtua wakurugenzi wa Google na kuwapelekea wafanye maamuzi ya haraka ya kuunda Bard, jibu lao kwa ChatGPT.

Google walizindua Bard mnamo Februari 2023, Bard ilipata kipaumbele zaidi baada ya hotuba kuu ya Google I/O iliyofanyika mwezi Mei. [1]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Bard (chatbot)", Wikipedia (kwa Kiingereza), 2024-01-10, iliwekwa mnamo 2024-01-11 
Makala hii kuhusu mambo ya teknolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hiyo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.