Bamia
Mandhari
Mabamia (kutoka jina la Kiarabu) au mabinda (kutoka jina la Kihindi) ni matunda ya mbamia au mbinda unaokuzwa sana katika nchi za joto.
Asili ya mboga hii ni Afrika ya Kati na Afrika ya Mashariki, lakini kwa sasa zao hili limeenea katika sehemu nyingi za kitropiki, kama Visiwa vya Karibi, Malaysia na Ufilipino.
Zipo aina nyingi za bamia, aina zile za asili nazo hutofautiana kulingana na eneo moja na lingine.
Zao hili hutumika kama mboga inayoliwa matunda, na kama kiungo katika mapishi mbalimbali.
Makala hii kuhusu mambo ya biolojia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Bamia kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |