Ashok Jivraj Rabheru

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru


Sir
Ashok Jivraj Rabheru

Kigezo:Post-nominals

Sir Ashok Jivraj Rabheru (6 Aprili 1952 - 23 Desemba 2022) alikuwa mfanyabiashara nchini Uingereza. Alikuwa mwenyekiti wa Kampuni ya Tekonolojia na mawasiliano, inayoitwa Genisys Group. [1] Alihudumu kama mdhamini wa Tuzo ya Duke of Edinburgh kuanza mwaka 2000 hadi 2010, na alikuwa mwanachama mkuu wa kikundi cha uongozi kwa ajili ya kukusanya fedha kwa ya maadhimisho ya Jubilee ya Dhahabu mwaka wa 2006. [2] Alikuwa mwenyekiti wa bodi ya pamoja ya ufadhili kwa Uingereza na shughuli za kimataifa.

Maisha ya awali na elimu[hariri | hariri chanzo]

Rabheru alizaliwa mkoani Morogoro, Tanzania, alikuwa mtoto wa tisa kati ya kumi wa Raliat na Jivraj. Baba yake alizaliwa na aliktoka India. [3]

Mnamo mwaka 1967, Rabheru alihama nchini Uingereza akiwa na umri wa miaka 15. Rabheru alisoma Chuo cha Kingston na kupata digrii yake kutoka Chuo Kikuu cha London katika ( B.Sc. ). Pia alishikilia ( M.Phil. ) kutoka Royal Holloway, Chuo Kikuu cha London katika Applied Mathematics. [3]

Kazi[hariri | hariri chanzo]

Rabheru alianza taaluma yake ya TEHAMA kwa kuunda kampuni ya Genisys Group [4] mwaka wa 1985, Alikuwa na wafanyakazi 5 tu na leo kampuni hiyo imekua mtoa huduma za IT kwa kimataifa ikiwa na wafanyakazi zaidi ya watu 1000. Katika miongo mitatu iliyopita, kampuni imesaidia biashara kufikiria upya biashara zao katika ulimwengu wa kidijitali, kwa kutoa masuluhisho ya kina ya teknolojia yanayoungwa mkono na uzoefu, kujitolea na mkakati.

Maisha ya kibinafsi na kifo[hariri | hariri chanzo]

Rabheru alikuwa na mke, Harshida Jivraj Rabheru, alikutanae wakati walikuwa na soma katika Chuo cha Kingston na walifunga ndoa mwaka wa 1980 nchini Kenya [5] [3] . Wali bahatika kupata watoto watatu mapacha: Rishi, Shayan na Nikita, na aliishi Buckinghamshire. [6]

Rabheru alifariki tarehe 23 Desemba 2022, akiwa na umri wa miaka 70. [3]

  1. "About Genisys: Who we are, what we do, how we do it". Genisys Group. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 18 September 2021. Iliwekwa mnamo 7 October 2023.  Check date values in: |archivedate=, |accessdate= (help)
  2. "Ashok J Rabheru CVO DL – The Duke of Edinburgh's Award". www.dofe.org (kwa en-US). Iliwekwa mnamo 2018-07-09. 
  3. 3.0 3.1 3.2 3.3 Bhat, Chandrashekar (25 December 2022). "Genisys Group founder Sir Ashok Rabheru, 70, dies". EasternEye.  Check date values in: |date= (help) Hitilafu ya kutaja: Invalid <ref> tag; name "Death" defined multiple times with different content
  4. "Genisys Group | IT, Software Development, Business Process Services". Genisys Group (kwa en-US). Iliwekwa mnamo 2022-05-12. 
  5. "Asian Voice". 
  6. "Ashok Jivraj Rabheru". Women Economic Forum. Iliwekwa mnamo 7 October 2023.  Check date values in: |accessdate= (help)