Arudhi
Arudhi katika fasihi ni sehemu muhimu katika elimu ya utunzi wa mashairi. Hasa arudhi inaelezea vipengele vya mashairi kama beti, idadi ya mishororo, vina na mizani.
Arudhi katika isimu inahusu vipengele vya mabadiliko ya vipambasauti, k.m. kidatu, nguvumsikiko au lahani.
Marejeo [hariri]
- Massamba, David 2004, "Kamusi ya Isimu na Falsafa ya Lugha", Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
- Oriedo, Hannington 2007, "Istilahi za Fasihi ya Kiswahili", Nairobi: Kenya Literature Bureau
- Wamitila, Kyallo 2003, “Kamusi ya Fasihi – Istilahi na Nadharia”, Nairobi: Focus Books
Tazama pia [hariri]
Viambishi ni mofimu au viungo vyenye maana ambavyo hufungamanishwa na mzizi/shina la neno ili kulipa neno hilo maana mbalimbali za kisarufi kama vile nafsi, wakati, hali, urejeshi, n.k Viambishi awali ni vile vinavyotangulia mzizi wenyewe, yaani huwa kabla ya mzizi/shina. SHINA AU MZIZI: Hakuna tofauti kati ya shina na mzizi MZIZI/SHINA, Ni sehemu ya neno inayobeba maana yake kuu na huwa haibadiliki, Kwa mfano, tuangalie vitenzi vifuatavyo: a-na-LIM-a wa-li-LIM-i-a ni-ta-LIM-iw-a wa-na-vyo-LIM-a Ukiangalia kwa makini, utaona kuna sehemu ya kitenzi hiki ambayo haibadiliki katika mifano ya hapo juu. Sehemu hiyo ni (-LIM-). Na hii ndiyo shina au mzizi wa kitenzi LIMA. Mfano mwingine: a-li-ki-SOM-a hu-SOM-ew-a wa-li-SOM-e-an-a a-li-m-SOM-e-a i-li-SOM-w-a Tunaona hapa mzizi/shina la kitenzi SOMA, ni -som- Ili utambue shina/mzizi wa kitenzi unafaa kuwazia hali mbalimbali au kauli tofautitofauti za mnyambuliko wa kitenzi halafu ubainishe sehemu isiyobadilika.