Angèle Bandou

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Angèle Bandou (alifariki Agosti 26, 2004) alikuwa mwanasiasa katika Jamhuri ya Kongo. Alikuwa mwanzilishi na Rais wa chama cha Maskini (Kongo-Brazzaville). Alikuwa mgombea pekee wa kike katika Uchaguzi wa Rais wa Kongo wa mwaka 1992, na uchaguzi uliofuata wa mwaka wa 2002 ambapo alimaliza wa tatu. Bandou alikuwa mwanamke wa kwanza kugombea Urais katika Jamhuri ya Kongo. Alikuwa ameuawa na watu wasiojulikana nyumbani kwake mwaka wa 2004.

Kazi ya Kisiasa[hariri | hariri chanzo]

Alianzisha Chama cha Maskini (Jamhuri ya Kongo) mwaka 1991.[1] Bandou alikuwa mtawa, ambaye alisema kwamba kuingia katika siasa ilikuwa ni wito kutoka kwa Mungu, akifafanua kwamba Mungu aliniambia niunde chama na akaniambia itakuwa mapinduzi ya pili katika nchi yetu. Wakati wa ujumbe huo, hapakuwa na mchakato wa kidemokrasia chini ya serikali ya Marxist. Alijitokeza katika Uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya Kongo mwaka 1992 kwa niaba ya chama ambapo alipata chini ya asilimia moja ya kura kwa jumla.[1] Bandou alisema kujibu idadi ndogo ya kura alizopokea, Macho ya binadamu, nilishindwa. Lakini kiroho, nilileta ujumbe. Kwa kugombea mwaka 1992, yeye alikuwa mwanamke wa kwanza kugombea urais katika nchi hiyo.

Alijitahidi kugombea tena katika uchaguzi wa mwaka 1997 ambao uliahirishwa, badala yake alisimama katika Uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya Kongo mwaka 2002 kama mmoja wa wagombea kumi.[2] Alipokea kura 27,849 (asilimia 2.32) akimaliza nafasi ya tatu nyuma ya Joseph Kignoumbi Kia Mboungou wa Umoja wa Afrika kwa Demokrasia ya Kijamii (kura 33,154, asilimia 2.76) na Rais wa baadaye Denis Sassou Nguesso wa Chama cha Wafanyakazi wa Kongo (kura 1,075,247, asilimia 89.41).

Katika mahojiano mwaka 1997, alieleza kwamba mtazamo wake kuhusu siasa ulitegemea kufanya kazi na vijana wa nchi na Afrika kwa ujumla, pamoja na kuboresha elimu. Bandou alihisi kwamba wanawake zaidi wanapaswa kushiriki katika siasa, akisema kwamba mila inadai majukumu ya wanaume na wanawake katika jamii, pamoja na kuongeza njia ambayo siasa inavyofanyika Afrika inawatisha wanawake... vijana wanapewa silaha, watu wanauana... Nahitaji kukiri kwamba kama Mungu asingenipa jukumu hili, singethubutu kugombea.

Kifo[hariri | hariri chanzo]

Tarehe 26 Agosti 2004, Angèle Bandou aliuawa na watu wasiojulikana nyumbani kwake. Uvumi ulienea kwamba mauaji yalifanywa kwa amri ya Rais Nguesso.[1]


Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. 1.0 1.1 1.2 Clark, John Frank (2012). Historical Dictionary of Republic of the Congo. Lanham: Scarecrow Press. uk. 57. ISBN 978-081-084-919-8. 
  2. "Election présidentielle au Congo Brazzaville : Un processus électoral contesté par l'opposition", rfi, 21 February 2002. Retrieved on 8 November 2016. (French) 
Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Angèle Bandou kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.