Alumniportal Deutschland

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Nembo ya Alumniportal Deutschland

Alumniportal Deutschland (Mlango wa Alumni Ujerumani) ni ukurasa kwenye mtandao. Madhumuni yake ni kuwaunganisha Alumni wa Ujerumani. Alumni-Ujerumani ni watu wote duniani ambao walisomea, waliofanya kazi, utafiti, waliosoma lugha ama kwa kusafiri kwenda Ujerumani ama katika chuo chochote cha Ujerumani kwenye nchi za kigeni. Ukurasa huu watumika bila malipo na sio wa kibiashara. Huu ni mradi wa mashirika matano ya Ujerumani ya ushirikiano wa kimataifa. Fedha za mradi huu zinatoka katika Wizara ya ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo (Bundesministerium für wirtschaftliche Zusammenarbeit und Entwicklung, BMZ).

Wajibu na Madhumuni[hariri | hariri chanzo]

Ukurasa huu unawezesha uhusiano kati ya Alumni wa kijerumani na Ujerumani. Alumni-Ujerumani wanaweza kuwasiliana wenyewe kwa wenyewe, kuwasiliana na mashirika ya Ujerumani pamoja na yale ya kimataifa, makampuni, vyuo vikuu, kujenga na kufafanua mitandao ya Alumni. Ukurasa huu una soko la kazi na unatoa habari kuhusu kazi za kimataifa, habari kuhusu nafasi za kuendeleza masomo, habari za matukio kote duniani, sehemu ya tahariri yenye makala ya utamaduni, jamii, elimu sayansi & utafiti na uchumi, sehemu ya lugha ya kijerumani yenye walimu wa kijerumani ambao wajitangaza pamoja na jamii. Ukurasa huu ni wazi kwa Alumni wote bila kujali kama unajilipia gharama za maisha mwenyewe ama unalipiwa na shirika fulani la Ujerumani.

Mtandao huu mkubwa wa mawasiliano unawezesha mashirika ambayo yanahusika katika kujenga ushirikiano bora zaidi kwa kazi zao za Alumni. Ukurasa huu unaunganisha biashara na waajiri, watalamu ama wabia wa kibiashara.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Kazi ya Alumni yaani kufanya kazi na wanafunzi wa zamani wa chuo fulani cha masomo ya ngazi za juu kwa kawaida yafanyika kwenye mashirika ambayo yanawafadhili Alumni.

Kama asilimia 80 ya wanafunzi wa kigeni, ambao wanasomea Ujerumani, yaani watu 14,000 kwa mwaka, walijilipia karo ya masomo yao, na ni vigumu sana kupata kujua anwani zao. Hivyo ndivyo ukurasa huu wa mtandao-Ujerumani ulivyoanzishwa. Huu ni ukurasa wa kipekee ambao unaunganisha kazi ya Alumni wa Ujerumani, ustadi wao pamoja na kuwaunganisha Alumni wenyewe, kwa manufaa ya mashirika ambayo yanawafadhili Alumni, na kwa manufaa ya mashirika yote duniani ambayo yanahitaji wafanyikazi. Mpaka Julai 2011 watu wapatao 32,000 kutoka nchi 184 walikuwa wamejiandikisha kama watumiaji wa ukurasa huu.

Muundo[hariri | hariri chanzo]

Kitu chenye umuhimu zaidi kwa ukurasa huu ni ‘online community’. Ili uweze kutumia ukurasa huu unahitaji kujiandikisha. Unajiandikisha bila malipo. Alumni wanaweza kuwasiliana wao kwa wao ama kuwasiliana na makampuni. Pia kuna uwezekano wa kuanzisha na kutumia Blogs. Ukurasa huu una maktaba ya habari ambayo inawapasha Alumni habari kuhusu nafasi mbalimbali za mada na inaleta hamu kwa jamii. Hizi ni nafasi kama vile soko la kazi za kimataifa na soko la mikataba ya kazi, kalenda ya matukio, nafasi za kusoma Kijerumani, nafasi za kusomea utaalamu wa nyanja mbalimbali, huduma za uhariri na mengineo kutokana na uwanja wa uchumi, utafiti, sayansi, na utamaduni. Mashirika ama makampuni yanaweza kutuma kazi ambazo wanazo kwa soko la kazi. Wanaweza pia kutafuta wafanyakazi katika benki ya data, kutoa habari kuhusu matukio ama kutafuta wataalamu wanaowahitaji. Ukurasa huu wa Alumni Ujerumani umeandikwa kwa lugha ya Kijerumani na Kiingereza.

Wafadhili na wabia[hariri | hariri chanzo]

Alumni Ujerumani ni mradi wa mashirika mablimbali na masomo mbalimbali. Ni mradi wa mashirika matano ya ushirikiano wa kimataifa.

Zaidi ya wabia kumi muhimu sana wanauunga mkono ushirikiano huu kwa mfano wizara ya mambo ya kigeni, wizaza ya masomo na utafiti, mifuko tofauti ya kisiasa ya kama vile Friedrich Ebert Foundation, Konrad Adenauer Foundation na Heinrich Boell Foundation.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]