Alice Muloki

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Alice Muloki (19 Novemba 1929 - 6 Novemba 2005) alikuwa Inhebantu (malkia mke) wa Ufalme wa Busoga huko Uganda[1] kwa kuolewa na Henry Wako Muloki, mtawala wa ufalme huo, ambaye alijulikana kama Kyabazinga wa Busoga.[2]

Maisha ya awali na elimu[hariri | hariri chanzo]

Muloki alizaliwa kama Alice Kintu mnamo Novemba 19, 1929. Alipata elimu katika shule ya Berkley High School, Gayaza High School na Chuo cha Buloba huko Busoga.[1] Kisha alipata mafunzo ya kuwa mwalimu wa Darasa la 3 katika [huo cha Walimu cha Msingi cha Buloba karibu na Kampala, baada ya hapo alifundisha katika Shule ya Buckley High School, kabla ya kuhamishiwa kufanya kazi huko Kamuli. Mwaka 1956, alijiuzulu kutoka kwenye kazi ya kuwa mkuu wa Chuo cha Walimu cha Msingi cha Bishop Willis Core.

Maisha yake binafsi[hariri | hariri chanzo]

Alice Muloki aliolewa na Kyabazinga Henry Wako Muloki mnamo Januari 21, 1956.[3] Wapenzi hao walikuwa na watoto nane pamoja[4]-wakiume wanne na mabinti wanne.[3]

Muloki alikuwa mtetezi hodari wa mipango ya Elimu kwa Mtoto wa Kike, na mipango mingine mbalimbali katika Busoga.

Alice Muloki alifariki mnamo Novemba 6, 2005.[3] Alizikwa katika Wilaya ya Kaliro. Mume wake, Henry Wako Muloki, alizikwa[5] pamoja naye huko Kaliro baada ya kifo chake mnamo mwaka 2008.[3]

Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Alice Muloki kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. 1.0 1.1 "Alice Muloki". www.wikidata.org (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2020-05-30. 
  2. "The life and times of Kyabazinga Muloki". www.newvision.co.ug. Iliwekwa mnamo 2019-06-01. 
  3. 3.0 3.1 3.2 3.3 Bita, George. "Life and times of Wako Muloki", New Vision, 2008-09-14. Retrieved on 2008-09-26. Archived from the original on 2008-09-02. 
  4. "Proud Musoga". www.proudmusoga.co.ug. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-06-01. Iliwekwa mnamo 2019-06-01. 
  5. "Life and times of Wako Muloki". www.newvision.co.ug. Iliwekwa mnamo 2019-06-01.