Neopalpa donaldtrumpi : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
Ukurasa ulianzishwa kwa kuandika '{{Italic title}} {{Taxobox | name = ''Neopalpa donaldtrumpi'' | image = Close up photograph of the Head of a Male Neopalpa donaldtrumpi.jpg | image_caption = Ki...'
(Hakuna tofauti)

Pitio la 19:42, 21 Januari 2017

Neopalpa donaldtrumpi
Kichwa cha Neopalpa donaldtrumpi kwa kuitazama kutoka upande wa kushoto na mbele.
Scientific classification
Kingdom: Animalia
Phylum: Arthropoda
Class: Insecta
Order: Lepidoptera
Family: Gelechiidae
Genus: Neopalpa
Species: N. donaldtrumpi
Binomial name
Neopalpa donaldtrumpi
Nazari, 2017

Neopalpa donaldtrumpi ni spishi ya kipepeo iliyogunduliwa mwaka 2017 na mtaalamu wa Kanada Vazrick Nazari. Akiwa mgunduzi wa spishi mpya Nazari aliweza kuchagua jina akaamua kutumia jina la mwanabiashara na wakati ule mgombea wa uraisi Donald Trump kwa matumaini ya kwamba chaguo hili litasababisha watu wengi zaidi kusikia habari za wadudu na utafiti wa wadudu.

Ugunduzi

Donald Trump akionyesha nywele zake za ajabu

Jenasi Neopalpa pamoja na spishi Neopalpa neonata ilielezwa mara ya kwanza mwaka 1998 by Dalibor Povolný.[1] Miaka 20 baadaye Vazrick Nazari aliangalia upya mifano ya kipepeo hiki iliyohifadhiwa katika taasisi ya Bohart Museum of Entomology.[2] Alitambua ya kwamba mifano kadhaa ilitofautiana na mingine na kuwa spishi mpya aliyoiita Neopalpa donaldtrumpi kwa sababu ya magamba ya rangi ya njano - nyeupe kichwani. Haya yalimkumbusha kuhusu nywele za Donald Trump.[3] Ilhali nafasi yake ya kueleza spichi mpyza ilitokea karibu na tarehe ya Trump kuingia katika uraisi kwenye Januari 2017 aliamua kutumia hili kwa sababu aliona sayansi ya wadudu ilihitaji kujulikana zaidi.[3][4]

Tabia

Mwili wa kipepeo hiki una urefu baina ya milimita 7 na 13. Mabawa yake hufunika upana wa milimita 6 hadi 9.2. Uso wa juu wa mabawa huwa na rangi kahawia pamoja na madoa meupe zaidi. Kichwa kina magamba meupe-njano yaliyosababisha uteuzi wa jina.[3][4] Pamoja na magamba ya kichwani tofauti nyingine ya spishi hii na spishi ya N. neonata ni udogo wa mboo na pia umbo la sehemu za kike. Zinatofautishwa pia kutokana na DNA.[3]

Habitat

Hadi sasa Neopalpa donaldtrumpi ilionekana kwenye sehemu za kaskazini ya rasi ya Baja California katika Meksiko na kwenye kaskazini ya Kalifornia ya Marekani.[3]


Marejeo

  1. Povolný, Dalibor. "Neopalpa gen. n. and Eurysaccoides gen. n. — two new genera of the tribe Gnorimoschemini from California, with the description of three new species (Lepidoptera, Gelechiidae)". Revista de Lepidopterología (Sociedad Hispano-Luso-Americana de Lepidopterología) 26: 139–146. 
  2. Fitch, Chris. "Meet the Trump moth", Royal Geographical Society, 2017-01-18. 
  3. 3.0 3.1 3.2 3.3 3.4 Nazari, Vazrick (2017). "Review of Neopalpa Povolný, 1998 with description of a new species from California and Baja California, Mexico (Lepidoptera, Gelechiidae)". ZooKeys 646: 79. doi:10.3897/zookeys.646.11411. 
  4. 4.0 4.1 "Neopalpa donaldtrumpi Motte trägt nun Namen von Donald Trump". Spiegel Online, 18 January 2017 (German)

Viungo vya Nje

Wikimedia Commons ina media kuhusu: