Chanjo ya kipindupindu : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
from English (EN) Wikipedia and Medical Translation Task Force with help from Translators Without Borders (human translation). CC-BY-SA
(Hakuna tofauti)

Pitio la 17:19, 3 Mei 2016

Chanjo ya kipindupindu ni chanjo madhubuti katika kuzuia kipindupindu.[1] Zinatenda vizuri 85% muda wa miezi sita wa kwanza na 50-60% muda wa mwaka wa kwanza. [1][2][3] Uponaji wake unapungua hadi kasoro 50% baada ya muda wa miaka miwili. Endapo asilimia kubwa ya idadi ya watu wa nchi moja imepata kinga madhubuti maslahi kutoka kwa kinga kuwepo kwa waliowengi pengine yanatokea miongoni mwa wale wasio na kinga madhubuti. Shirika la Afya Duniani linapendekeza matumizi yao pamoja na mkusanyo wa namna za tibu zingine kwa wale wenye hatari kubwa ya kuambukizwa.<!—ref name=WHO2010/> Dozi mbili au tatu ya aina ya kumezwa kwa kawaida zinapendekezwa. [1] Aina ya kudungwa na sindano inapatikana maeneo mengine ya dunia bali upatakanaji wake si sawa na ile ya kumezwa. [2][1]

Usalama

Aina zote mbili za chanjo za kumezwa hazina hatari ni salama.[1] Maumivu yasiyo kali ya fumbatio au kuharisha huenda yatatokea. Ni salama kwa akina mama wajaa wazito pamoa na wenye utendaji mbovu wa kingamwili. Zinasajiliwa kutendeka katika nchi zaidi ya 60. Zinatumika katika nchi ambako maradhi hutokea kwa wingi na bei ni nafuu. [1]

Jamii na utamaduni

Chanjo za kwanza zilizotumiwa dhidi ya kipindupindu ziliundwa katika enzi za mwisho za 1880. Zilikuwa za kwanza kutumiwa katika maeneo mengi ya dunia ambazo zilitengenezwa katika maabara. [4] Chanjo za kumezwa zilitumiwa kwa mara ya kwanza katika enzi za 1990.[1] Ipo kwenye Orodha ya Dawa Muhimu ya Shirika la Afya Duniani, dawa muhimu sana katika mfumo wa afya.[5] Bei ya ukingaji dhidi ya kipindupindu iko kati ya 0.1 na 4.0 sarafu ya Marekani [6]

Marejeo

  1. 1.0 1.1 1.2 1.3 1.4 1.5 1.6 "Cholera vaccines: WHO position paper.". Weekly epidemiological record 13 (85): 117–128. Mar 26, 2010. PMID 20349546. 
  2. 2.0 2.1 Graves PM, Deeks JJ, Demicheli V, Jefferson T (2010). "Vaccines for preventing cholera: killed whole cell or other subunit vaccines (injected)". Cochrane Database Syst Rev (8): CD000974. PMID 20687062. doi:10.1002/14651858.CD000974.pub2. 
  3. Sinclair D, Abba K, Zaman K, Qadri F, Graves PM (2011). "Oral vaccines for preventing cholera". Cochrane Database Syst Rev (3): CD008603. PMID 21412922. doi:10.1002/14651858.CD008603.pub2. 
  4. Stanberry, Lawrence R. (2009). Vaccines for biodefense and emerging and neglected diseases (toleo la 1). Amsterdam: Academic. uk. 870. ISBN 9780080919027. 
  5. "WHO Model List of EssentialMedicines". World Health Organization. October 2013. Iliwekwa mnamo 22 April 2014.  Check date values in: |date=, |accessdate= (help)
  6. Martin, S; Lopez, AL; Bellos, A; Deen, J; Ali, M; Alberti, K; Anh, DD; Costa, A; Grais, RF; Legros, D; Luquero, FJ; Ghai, MB; Perea, W; Sack, DA (1 December 2014). "Post-licensure deployment of oral cholera vaccines: a systematic review.". Bulletin of the World Health Organization 92 (12): 881–93. PMID 25552772.  Check date values in: |date= (help)