Pepopunda : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
from English (EN) Wikipedia and Medical Translation Task Force with help from Translators Without Borders (human translation). CC-BY-SA
(Hakuna tofauti)

Pitio la 19:01, 10 Machi 2016

Tetanasi
Mwainisho na taarifa za nje
ICD-10A33.-A35.
ICD-9037, 771.3
DiseasesDB2829
MedlinePlus000615
eMedicineemerg/574
MeSHD013742

Tetanasi, pia iitwayo pepopunda, ni maambukizi yaliyo na sifa bainifu ya mvutano wa misuli. Katika aina ya kawaida sana mivutano huanza kwenye taya na kisha kuenea kwenye sehemu nyingine ya mwili. Mivutano hii kwa kawaida hudumu kwa muda wa dakika chache kila wakati na hutokea mara kwa mara kwa wiki tatu hadi nne.[1] Mivutano inaweza kuwa kali sana ambapo kuvunjika kwa mifupa kunaweza kutokea.[2] Dalili zingine zinaweza kujumuisha: joto jingi, maumivu ya kichwa, tatizo la kumeza, shinikizo la damu, na mpigo wa haraka wa moyo.[1][2] Kuanza kwa dalili kwa kawaida huwa siku tatu hadi ishirini na moja baada ya maambukizi. Unaweza kuchukua miezi kabla ya kupona. Takribani asilimia 10 ya walioambukizwa hufariki.[1]

Kisababishi na utambuzi

Pepopunda husababishwa na maambukizi yaliyo na bakteria Kostridiamu tetani.[1] Kwa kawaida bakteria huingia mwilini kupitia mwanya kwenye ngozi kama vile mahali palipokatwa au jeraha lililosababishwa na kifaa chafu. Bakteria hizi hupatikana kwa kawaida kwenye udongo, vumbi na mbolea.[3] Bakteria hutoa toksini inayotatiza mikakamao ya misuli, huku ikisababisha dalili za kawaida.[4] Utambuzi huzingatia misingi ya ishara na dalili. Hugonjwa huu hauenei kati ya watu.[1]

Uzuiaji, matibabu na prognosisi

Maambukizi yanaweza kuzuiwa kwa uchanjaji bora kwa chanjo ya pepopunda. Kwa wale walio na kidonda kubwa na chini ya dozi tatu za chanjo uchanjaji na globulini ya kinga dhidi ya pepopunda hupendekezwa. Kwa walioambukizwa globulini ya kinga dhidi ya pepopunda au iwapo haipatikani imunoglubolini ya kudunga mishipani (IVIG) hutumika. Kidonda kinapaswa kuoshwa na kila tishu iliyokufa kuondolewa.[1] dawa ya kulegeza misuli inaweza kutumika ili kudhibiti mivutano. tundu lililoandaliwa la kupitisha hewa mlinaweza kuhitajika iwapo kupumua kwa mtu kumeathirika.[4]

Epidemiolojia na historia

Pepopunda hutokea katika sehemu zote za dunia lakini hutokea mara nyingi zaidi katika hali ya anga iliyo joto na iliyo na unyevunyevu pale ambapo udongo huwa na viumbe hai.[1] Katika mwaka wa 2013 ilisababisha takribani vifo 59,000 – idadi iliyopungua kutoka 356,000 katika mwaka wa 1990.[5] Maelezo ya ugonjwa huu na Hippocrates yamekuwa kutoka angalau karne ya 5 BCE. Kisababishi cha ugonjwa kiligunduliwa katika mwaka wa 1884 huku chanjo ikianzishwa katika mwaka wa 1924.[1]

Marejeo

  1. 1.0 1.1 1.2 1.3 1.4 1.5 1.6 1.7 Atkinson, William (May 2012). Tetanus Epidemiology and Prevention of Vaccine-Preventable Diseases (toleo la 12). Public Health Foundation. ku. 291–300. ISBN 9780983263135. Iliwekwa mnamo 12 February 2015.  Check date values in: |date=, |accessdate= (help)
  2. 2.0 2.1 "Tetanus Symptoms and Complications". cdc.gov. January 9, 2013. Iliwekwa mnamo 12 February 2015.  Check date values in: |date=, |accessdate= (help)
  3. "Tetanus Causes and Transmission". www.cdc.gov. January 9, 2013. Iliwekwa mnamo 12 February 2015.  Check date values in: |date=, |accessdate= (help)
  4. 4.0 4.1 "Tetanus For Clinicians". cdc.gov. January 9, 2013. Iliwekwa mnamo 12 February 2015.  Check date values in: |date=, |accessdate= (help)
  5. GBD 2013 Mortality and Causes of Death, Collaborators (17 December 2014). "Global, regional, and national age-sex specific all-cause and cause-specific mortality for 240 causes of death, 1990-2013: a systematic analysis for the Global Burden of Disease Study 2013.". Lancet 385 (9963): 117–71. PMID 25530442. doi:10.1016/S0140-6736(14)61682-2.  Check date values in: |date= (help)