Tatizo la kutojizuia kurudiarudia tendo : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
Ukurasa ulianzishwa kwa kuandika '{{hatnote|"OCD" redirects here. For other uses, see OCD (disambiguation). Not to be confused with Obsessive–compulsive personality disorder.}} {{pp-mo...'
(Hakuna tofauti)

Pitio la 12:41, 12 Desemba 2018

Kigezo:Use American English Kigezo:Infobox medical condition (new) Tatizo la kiakili linalomfanya mtu kuwa na hofu na kisha kurudia tabia fulani (OCD) ni tatizo la kiakili ambapo huhisi haja ya kuangalia vitu mara kwa mara, tenda utaratibu fulani mara kwa mara (unaoitwa "matambiko"), au wana mawazo fulani mara kwa mara(yanayoitwa "shauku").[1] Watu hawana uwezo wa kudhibiti ama mawazo au shughuli kwa zaidi ya kipindi kifupi cha wakati.[1] Shughuli za kawaida ni kama vile kuosha mkono, kuhesabu vitu, na kuangalia kuona iwapo mlango umefungwa.[1] Wengine wanaweza kuwa na ugumu wa kutupa vitu nje.[1] Shughuli hizi hutokea kwa kiasi fulani kwamba maisha ya mtu ya kila siku inaathiriwa vibaya.[1] Hii mara nyingi hutokea zaidi ya saa moja kwa siku.[2] Watu wazima wengi hugundua kwamba tabia hizo hazina maana.[1] Hali hiyo inahusiana na mitetemo ya kineva, tatizo la kiakili linalosababisha wasiwasi kila mara, na kuongezeka kwa hatari ya kujitia kitanzi.[2][3]

Chanzo hakijulikani.[1] Kunaonekana kuwa na vijenzi fulani vya jenetiki na pacha wanaofanana kuathiriwa sana mara nyingi kuliko pacha wasiofanana.[2] Vipengele vya hatari ni kama vile historia ya unyanyasaji wa mtoto au tukiolinalosababisha mawazo.[2] Baadhi ya hali zimeshawekwa kwenye kumbukumbu kutokea kwa sababu ya maambukizi.[2] Utambuzi unategemea dalili na huhitaji kuondoa vyanzo vingine vinavyohusiana na dawa au matibabu.[2] Vipimo vya viwango kama vile Yale–Brown Obsessive Compulsive Scale (Y-BOCS) vinaweza kutumika ili kutathmini ukali wake.[4] Matatizo mengine yaliyo na dalili sawa ni pamoja na tatizo la kiakili linalosababisha wasiwasi kila mara, tatizo la kiakili linalosababisha huzuni kali kwa muda mrefu,tatizo la kiakili linalosababisha tabia ya kula isiyo ya kawaida, tatizo la kiakili linalosababisha mtetemo wa kineva usoni, na tatizo la kiakili linalomfanya mtu kuwa na hofu na kisha kurudia tabia fulani ya kibinafsi.[2]

Matibabu yanajumuisha ushauri, kama vile tiba ya tabia za utambuzi (CBT), na wakati mwingine dawa za kutibu huzuni kama vile kuchagua kizuizi cha ufyonyaji upya wa serotonini (SSRIs) au dawa ya kutibu matatizo ya hofu, wasiwasi na huzuni (clomipramine).[5][6] Tiba ya tabia za utambuzi (CBT) kwa Tatizo la kiakili linalomfanya mtu kuwa na hofu na kisha kurudia tabia fulani (OCD) huhusisha kuongeza kuwekwa wazi kwa chanzo cha shida huku huruhusu tabia ya kujirudia kutotokea.[5] Huku dawa ya kutibu matatizo ya hofu, wasiwasi na huzuni (clomipramine) huonekana kufanya kazi sawa na kuchagua kizuizi cha ufyonyaji upya wa serotonini (SSRIs), ina madhara mengi hivyo huhifadhiwa ili itumike kukihitajika.[5] Dawa za kutibu magonjwa ya kisaikolijia zisizo za kawaida zinaweza kuwa muhimu zikitumika pamoja na SSRI katika hali za kukataa matibabu lakini pia zinahusishwa na hatari ya ongezeko la madhara.[6][7] Bila matibabu, hali hiyo mara nyingi hudumu kwa miongo.[2]

Tatizo la kiakili linalomfanya mtu kuwa na hofu na kisha kurudia tabia fulani huathiri karibu 2.3% ya watu kwa wakati fulani maishani mwao.[8] Viwango katika mwaka fulani ni karibu 1.2%, na hutokea kote ulimwenguni.[2] Si kawaida kwa dalili kuanza baada ya umri wa miaka 35, na nusu ya watu huwa na matatizo kabla ya umri wa miaka 20.[1][2] wanaume na wanawake huathiriwa kwa viwango sawa.[1] Katika Kiingereza, kirai kuwa na hofu na kurudia kitu (obsessive-compulsive) mara nyingi hutumika kwa njia isiyo rasmi isiyohusika na Tatizo la kiakili linalomfanya mtu kuwa na hofu na kisha kurudia tabia fulani (OCD) kuelezea mtu ambaye mwangalifu sana katika mambo madogo madogo, mkamilifu, ametekwa fikra, au vinginevyo kufungwa kwa kitu au mtu.[9]


References

  1. 1.0 1.1 1.2 1.3 1.4 1.5 1.6 1.7 1.8 The National Institute of Mental Health (NIMH) (Januari 2016). "What is Obsessive-Compulsive Disorder (OCD)?". U.S. National Institutes of Health (NIH). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 23 Julai 2016. Iliwekwa mnamo 24 Julai 2016. {{cite web}}: Unknown parameter |deadurl= ignored (|url-status= suggested) (help)
  2. 2.00 2.01 2.02 2.03 2.04 2.05 2.06 2.07 2.08 2.09 Diagnostic and statistical manual of mental disorders : DSM-5 (toleo la 5). Washington: American Psychiatric Publishing. 2013. ku. 237–242. ISBN 978-0-89042-555-8.
  3. Angelakis, I; Gooding, P; Tarrier, N; Panagioti, M (25 Machi 2015). "Suicidality in obsessive compulsive disorder (OCD): A systematic review and meta-analysis". Clinical Psychology Review. 39: 1–15. doi:10.1016/j.cpr.2015.03.002. PMID 25875222.
  4. Fenske JN, Schwenk TL (Agosti 2009). "Obsessive compulsive disorder: diagnosis and management". Am Fam Physician. 80 (3): 239–45. PMID 19621834. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 12 Mei 2014. {{cite journal}}: Unknown parameter |deadurl= ignored (|url-status= suggested) (help)
  5. 5.0 5.1 5.2 Grant JE (14 Agosti 2014). "Clinical practice: Obsessive-compulsive disorder". The New England Journal of Medicine. 371 (7): 646–53. doi:10.1056/NEJMcp1402176. PMID 25119610.
  6. 6.0 6.1 Veale, D; Miles, S; Smallcombe, N; Ghezai, H; Goldacre, B; Hodsoll, J (29 Novemba 2014). "Atypical antipsychotic augmentation in SSRI treatment refractory obsessive-compulsive disorder: a systematic review and meta-analysis". BMC Psychiatry. 14: 317. doi:10.1186/s12888-014-0317-5. PMC 4262998. PMID 25432131.{{cite journal}}: CS1 maint: unflagged free DOI (link)
  7. Decloedt EH, Stein DJ (2010). "Current trends in drug treatment of obsessive-compulsive disorder". Neuropsychiatr Dis Treat. 6: 233–42. doi:10.2147/NDT.S3149. PMC 2877605. PMID 20520787.{{cite journal}}: CS1 maint: unflagged free DOI (link)
  8. Goodman, WK; Grice, DE; Lapidus, KA; Coffey, BJ (Septemba 2014). "Obsessive-compulsive disorder". The Psychiatric clinics of North America. 37 (3): 257–67. doi:10.1016/j.psc.2014.06.004. PMID 25150561.
  9. Bynum, W.F.; Porter, Roy; Shepherd, Michael (1985). "Obsessional Disorders: A Conceptual History. Terminological and Classificatory Issues.". The anatomy of madness : essays in the history of psychiatry. London: Routledge. ku. 166–187. ISBN 978-0-415-32382-6.

External links

Kigezo:Medical resources

Wikimedia Commons ina media kuhusu:

Kigezo:Obsessive–compulsive disorder Kigezo:OCD pharmacotherapies