Mtumiaji:Jabir johnson
Kigezo:Mwandishi wa habari Jabir Johnson Mking’imle (alizaliwa 17 Agosti 1984) ni mwandishi wa habari, mtangazaji na mpiga picha nchini Tanzania. Uandishi wa habari aliuanza mwaka 2008. Mashtaka ya kuendesha blogu pasipokuwa na leseni yaliyokuwa yakimkabili yalimalizika mnamo 22 Septemba 2021 baada ya mahakama kufuta mashtaka hayo.
Mnamo mwaka 2013 alianza kuandikia gazeti la kila siku nchini humo la Tanzania Daima ambalo nalo lilifutwa katika orodha ya magazeti wakati wa utawala wa Rais John Pombe Magufuli. Amewahi kufanya kazi na Redio Kili FM ya mkoani Kilimanjaro kwa vipindi viwili tofauti mnamo 2012-2013 na 2019 hadi Julai 31, 2020. Pia gazeti la Tanzania Daima (ambalo limerudishiwa leseni yake baada ya Rais Samia Suluhu kushika hatamu za uongozi)
Mnamo Aprili 2021 alipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Moshi kwa kuendesha blogu ya michezo na burudani inayofahamika kwa jina la Jaizmelaleo. Upande wa utetezi ulisimamiwa na wakili Ally Mhyellah kutoka Arusha.
Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) umeendelea kutoa msaada mkubwa wa kisheria kwa mwandishi huyo wa habari na wengine nchini humo wanaokabiliwa na mashtaka yanayofanana na hayo. THRDC inaendelea kulipigia kelele suala la sheria ya Huduma kwa Vyombo vya Habari ya mwaka 2016 ambayo bado inaendelea kuminya utoaji wa maoni.
Mnamo Aprili mwaka 2020, alikamatwa na Jeshi la Polisi na kushikiliwa kwa saa 37 akihojiwa na kitengo cha upelelezi kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani kisha kuachiwa kwa dhamana.