Tete (mji)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Picha ya daraja la kusimamishwa lenye urefu wa kilomita moja juu ya Mto Zambezi linalopatikan andani ya mji wa Tete ndani ya mkoa wa Tete
Mahali pa Tete nchini Msumbiji
Mahali pa Tete nchini Msumbiji

Tete ni mji mwenye wakazi 104,832 na makao makuu ya Mkoa wa Tete nchini Msumbiji. Iko kando la mto Zambezi takriban 420 km kutoka mdomo wake na mahali pa daraja mojawapo kati ya madaraja matano yanayovuka mto huu.

Tete ni mji wa kale uliojulikana kama kituo cha biashara cha Waswahili katika ufalme wa Mwene Mtapa. 1531 ilitwaliwa na Wareno ukawa kituo cha utawala wa Kireno katika bonde la Zambezi. Tangu karne ya 18 ilikuwa kituo cha kijeshi che Kireno na makao makuu ya utawala wa kikoloni wa eneo kubwa.

Hadi leo kuna majengo kadhaa za zamani za ukoloni pamoja na kanisa, hospitali na jumba la gavana. 32 km nje ya mji kuna misioni ya Boroma iliyoanzishwa na shirika la Yesu.

Siku hizi uchumi wa mji uko duni ingawa Tete imekuwa muhimu kwa mawasiliano ikiwa na daraja, kituo cha reli na uwanja wa ndege.