Shirika la Huduma za Maktaba Tanzania
Mandhari
Shirikia la Huduma za Maktaba Tanzania (kwa Kiingereza "Tanzania Library Services Board" au kifupi TLSB) lilianzishwa kisheria chini ya sheria za Tanzania iliyopitishwa na bunge mwaka 1972.
Shirika la Huduma za Maktaba Tanzania limekabidhiwa jukumu la kusimamia maendeleo ya huduma za maktaba Tanzania ikiwa ni pamoja na kutoa ushauri, kutoa mafunzo ya ukutubi kwa ngazi ya cheti na stashahada.
Shirika hili la umma linafanya kazi chini ya Wizara ya Elimu Tanzania na limesambaa katika mikoa yote Tanzania isipokuwa mkoa wa Singida peke yake. Lipo pia katika wilaya 33 za Tanzania bara.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Maktaba Tanzania Ilihifadhiwa 24 Januari 2021 kwenye Wayback Machine.
- OCLC WorldCat. National Central Library (Tanzania) Ilihifadhiwa 19 Agosti 2017 kwenye Wayback Machine.